Hivyo
tunaomba mtupostie kwenye blog zenu hili tangazo liwafikie watanzania
watakaopenda kumsaidia ili apelekwe Tanzania tutashukuru sana.
Tumefungua mahali pa kuchangisha hela http://www.donationto.com/adolfsendhomecost au
kama mtu anatumia paypal account ni adolffuneralcost@gmail.com.
Tutawapa majina ya watu watakaokua kwenye kamati ya kukusanya hela mara
tutakapomaliza kikao tunachotegemea kufanyika Jumamosi. na hela zote
zitaonyeshwa zilivyotumika kama zipo extra zitapelekwa huko kwa wajomba
zake Bukoba.
Na
kama kuna mtu ana picha yake basi mtutumie kwa sababu hakuna mtu aliye
na picha yake. ID yake ipo hospital hawawezi kumpa mtu mpaka wakishajua
nani anachukua mwili na mahali alipokua anaishi hawaruhusu mtu kuingia
kwa sasa mpaka wakishajua mazishi ni wapi au ndugu wa karibu ni wapi.
Hivyo hamna mtu ana picha yake..
Please
sisi hapa tunajitahidi ili azikwe kama ubinadamu hivyo huu sio muda wa
kuanza kuuliza maswali kwa nini hiki wala kile...Kwa vile hata sisi tuna
maswali mengi na hakuna mtu mweye jibu....Tunachojua ni kuwa alipata
massive stroke na amefariki na hakuna ndugu yake wa karibu huku
marekani.
Tunatanguliza
shukurani na pia kama blog yako hupost mambo ya habari tunaomba
utusaidie kuforward hii email kwa watu wengine...Kuna wazee wako NY kama
wakikukubali kushughulikia huu msiba tutawatangazia na kuwapa
information mpya. Na hela zitakazopatikana zitahamishiwa kwenye fund
yeyote watakayofungua kama wataamua kufungua mpya au wataamua kuendelea
na hi hii. Tunachotaka ni kusafirisha kijana wa watu Tanzania kwa sababu
sasa hivi hilo ndio lengo letu....na hakuna mtu yeyote aliyesema kitu
chochote hivyo
kama kikao kikifanyika basi tutawaeleza linaloendelea.
Nitajitahidi kuupdate kinachoendelea katika twitter handle yangu @swahilimom
Regards,
Pauline
0 comments:
Post a Comment