![]() |
| Inspector Henry akiwasihi mahabusu hao wawili wanaotuhumiwa kwa kesi za mauaji, kuachia mlingoti wa Bendera ya Taifa na kurudi kwenye chumba cha mahakama kwaajiri ya taratibu za kesi. |
![]() |
| Ushawishi ukiendelea. |
![]() |
| Mahabusu Thobiasi Warioba (aliye mtupu) pamoja na mwenzake Hamis Ramadhani katu katu waking'ang'ania mlingoti wa bendera ya Taifa huku wakishinikiza kuzungumza na waandishi wa Habari. |
![]() |
| Wananchi wamefurika viwanja vya mahakama. |
![]() |
| Baada ya kuzungumza na waandishi wa habari mahabusu hao walikubali kurejea chumba cha Mahakama. |
![]() |
| Nje ya Mahakama kuelekea lango kuu. |
![]() |
| Wananchi wamefurika viwanja vya mahakama. |
![]() |
| Mashuhuda. |
MAHABUSU wawili kati ya sita wanaotuhumiwa kwa kesi za mauaji, wameleta kizaazaa baada ya kujaribu kutoroka na kukimbilia kwenye mlingoti wa Bendera ya Taifa nakuing'ang'ania kisha kuvua nguo na mmoja wao kubaki mtupu.
Tukio hilo limetokea leo majira ya saa 4:00 asubuhi katika Mahakama ya Hakimu Mfawidhi wa Wilaya ya Nyamagana jijini Mwanza, wakati
mahabusu hao walipofikishwa kwa ajili ya kusikilizwa kwa kesi zao,
lakini ghafla walipofika kwenye viwanja vya mahakama hiyo walitimua
mbiyo kuelekea kwenye mlingoti wa Bendera hiyo ya Taifa na kuvua nguo.
Wananchi
waliokuwa katika viwanja vya mahakamani hapo waliachwa midomo wazi na
hali ya mshangao, mara baada ya mmoja kati ya hao wawili wakifanikiwa
kuufikia mlingoti huo na kuvua nguo kisha kuanza kupiga kelele kwa
kupaza sauti kudai haki itendeke.
Tukio
hilo pia lilishuhudiwa na watumishi wa Mahakama ya Wilaya, Mahakama ya
Mwanzo, Mamlaka ya Maji Safi na Majitaka ya jijini hapa (MWAUWASA),
Askari wa Jeshi la Wananchi (JWTZ), na taasisi zingine zilizo jirani na
majengo ya mahakamani hapo na wananchi waliokuwa wakisubilia kesi zao
kutajwa.
Mahabusu
hao sita waliojaribu kutoroka na kuishia kudhibitiwa vyombo vya dola,
walitajwa kwa majina kuwa ni Thobiasi Warioba (35), aliyeamua kuvua nguo
zote na kubaki mtupu eneo la mlingoti wa Bendera ya Taifa, ambaye
anakabiliwa na kesi ya mauaji Na. 32/2012.
Watuhumiwa
wengine waliojaribu kutoroka ni Hamis Ramadani (30), Anthony Petro
(35), Marwa Mwita (38), na Chacha Wangwe (35), na
mwingine ambaye hakufahamika majina yake mara moja, wote wanakabiliwa
na kesi ya Jinai Na. 215/2013 na walikamatwa tangu mwaka 2011.
Wakiwa
katika viwanja vya mahakama hiyo baada ya kudhibitiwa na askari polisi,
mmoja wa mahabusu hao walisikika wakisema: “Haiwezekani, tangu mwaka
2011 tulipokamatwa hadi sasa kesi zetu hazijasikilizwa. Wengine
tumebambikiziwa kesi. “Tunaomba haki zetu, polisi mnatuonea, vyombo vya habari tunaomba mtusaidie tumekaa
muda mrefu bila kusikilizwa na hatujui hatma yetu tangu 2011 tulipo
kamatwa tumechoka kukaa mahabusu, tunaomba kesi zetu zisikilizwe”.
Baada
ya malalamiko yao, ndipo
askari mmoja aliyejitambulisha kuwa ni Inspekta Henry akiwa na wenzake
sita waliokuwa wakiwadhibiti wasikimbie na kuwahoji kuhusiana na madai
yao, huku askari hao wakiwataka kuondoka katika mlingoti huo na kumtaka
Warioba avae nguo ili waweze kuingia mahakamani.
“Pamoja
na maamuzi yenu haya, lakini mtambue mnavunja sheria na hili ni kosa
jingine la jinai, hivyo ni vema mkaondoka kwenye mlingoti huu na kuingia
mahakamani. Malalamiko yenu tumeyasikia na yatashughulikiwa,” alisema
Inspekta Henry.
Mmoja
wa maofisa waandamizi wa Mahakama Kuu ya Tanzania Kanda ya Mwanza,
ambaye alikataa kutajwa jina lake, alidai ushahidi wa kesi za watuhumiwa
hao bado haujakamilika, na kwamba kesi zao haziwezi kusikilizwa na
mahakama ya wilaya kwani haina uwezo na badala yake zitatajwa tu kisha
kuhamishiwa Mahakama Kuu.
“Bado
hiyo ni Criminal Case (kesi ya mauaji) au PI Case hivyo Mahakama Kuu
haiwezi kuzungumzia hilo kwa sasa kwa kuwa utaratibu wa mahakama kuu
ikisha kuwa tayari huitwa ‘Criminary Session Case’, ambapo sasa
hupangiwa namba ya kesi na Jaji wa kuisikiliza,” alisema.











0 comments:
Post a Comment