Pages

Ads 468x60px

Friday, June 20, 2014

MWIMBAJI WA NYIMBO ZA INJILI DEBORA SAID AFARIKI DUNIA

Kwa kupitia Facebook Accout, Rais wa Chama cha Muziki wa Injili Tanzania Addo Novemba amepost habari za kifo cha mwimbaji wa nyimbo za Injili Tanzania Debora Said na hivi ndivyo alivyoandika, "Pigo Tena kwa Tasnia ya Muziki wa Injili, ninayo huzuni kubwa kuwatangazia Kifo cha Mwenzetu Deborah Said aliyefariki Muhimbili..naomba ushirikiano katika kipindi kigumu, kwa kuwa nipo nje ya Dar nikijiandaa kurudi nimeshamtuma Mhe Cosmas Chidumule aunganishe wanamuziki wote..Bwana Ametwaa, Tuonane Milele Tuonane Bandarini Pale!"
Marehem Debora Said enzi za uhai wake
Rumafrica imepokea kwa masikitiko makubwa sana juu ya kifo cha Debora, tunawapa pole wafiwa na Watanzania wote na kupotelewa na mtumishi wa Mungu ambaye amefanya kazi yake kwa upendo na uaminifu. Mungu azidi kuipigania familia yake na wale wote waliokuwa wakimtegemea kiroho na kimwili. Kazi ya Mungu daima haina makosa, tuzidi kumtumikia Mungu sisi tuliobaki kwani hatujui vilivyombele yetu.
 Huu ni wakati wa kuungama na kutubu makosa tunayoyafanya katika maisha yetu hapa dunia, siku ya mwisho tutatupwa jehanamu kama tukizidi kumsahau Mungu. Mungu amekupa kipaji fulani kwa kazi yake basi kitumia na usiache. Debora amefanya kazi ya Mungu kwa njia ya uimbaji na sasa Mungu amemchukua akampongezi kwa kile amekifanya duniani.

Dada Debora baada ya oparesheni



Hapa mama mchungaji, Debora John akimsifu Mungu, huku akienda sambamba na Mch. John Bagenyeka

0 comments:

Post a Comment