Mkutano
wafanyika katika ukumbi wa Paradise hotel jijini Mbeya,
kwa ufadhili
wa Society for Intrnational development (SID) na Foundation for civil Society (FCS)
Muwezeshaji wa warsha hiyo Edmund Matotay kutoka (SID) akitoa maelezo kwa washiliki
Monica Hangi Program Manager Society International Develpment (SID)![]() |
| Neema Yobu Program Manager Foundation For Civil society (FCS) |
Neema Yobu aliepo kulia na Monica Hangi wakiratibu mambo mbalimbali yanayohusu Warsha
Wana warsha wakisikiliza kwa makini kutoka kwa mkufunzi Edmund Matotay
Emile Malinza Regina Ngalawa Mwanafunzi (MNMA)
Alpha Laizer, Mwanafuzi wa chuo kikuu Teku
Christina Patrick Afisa mtendaji kata ya Itezi Jijini Mbeya
Eugen Kisonga Mkurugenzi Mbeya Hop for Ophans
Aggrey Kandonga, Mwenyekiti wa Mtandao wa mashirika yasiyo ya kiserikali wilaya ya Mbeya
Samwel Mbaule, Mwalimu shule ya sekondal Vanessa
Issa Mwasinyanga, Mchungaji wa kanisa la Baptist
Simon Mkaya, Mweka hazina Mbengonet
Baadhi ya wana warsha wakichangia maoni ya mada husika katika mkutano unaendelea katika ukumbi wa Paradise Hotel
Habari
Baadhi ya wana warsha wakichangia maoni ya mada husika katika mkutano unaendelea katika ukumbi wa Paradise Hotel
Habari
Baadhi ya wadau washiliki warsha kujadili
mustakabali wa Tazania mika 20 ijayo,
Mkutano
wafanyika katika ukumbi wa Paradise hotel jijini Mbeya,
kwa ufadhili
wa society for Intrnational development (SID) na Foundation for civil Society
Baadhi ya
wadau mkoani hapa wamekutana kataka warsha ya siku moja katika ukumbi wa
Paradise Hoteli uliopo maeneo ya Soweto kwa lengo la kujadiliana kuhusu
mustakabali wa Taifa la Tazania miaka 20
ijayo yaani hatima na mustakabali wa taifa ifikapo mwaka 2035
Katika
warsha hiyo Iliyoendeshwa na mkufunzi Edmund Matotay toka Socety International
Divelopment (SID) na kuratibiwa nae Neema Yobu wa Foundational for civil (FCS)
pamoja na Monica Hangi kutoka Society International.
Ililenga
kujadili nafasi ya Tanzania katika Shirikisho la Afrika mashariki, miundombinu
ya nchi, hali na mustakabali wa muungano wetu,mustakabali wa kilimo chetu na
mabadiliko ya nchi na athari zake.
Akiongea
mkufunzi wa walsha hiyo Matotay, amewataka washiriki kujadili na kupambanua
mustakabali wan chi yetu kwa miaka mingi ijayo lakini pia kuangali maswala
muhimu nay a msingi kama vile nini kimetusaidia nchi yetu kufikia hapa ilipo
leo.
Ameongeza
kua Tanzania itakuaje ifikapo mwaka 2035 nini kitafanya jamii yetu kubadilika
na nini kitatokea majadiliano hayo yaibue maono ya pamoja hata yale ya
kutofautiana lakini pia mwisho wa siku kuibua matumaini ya pamoja na
mustakabali wa Tanzania yetu ya baadae.
Wakijadili
mada hiyo makundi yalikua na maono mbalimbili kwa kujifikilisha ikiwemo Tanzania
ya miaka hiyo itakuana ufinyu wa fursa
na kuchochea uasi kwa wasio nacho kuchoshwa na umasikini wa kutupwa pia huduma
mbaya za kijamii.
Mambo mengine
ni kushindwa kulipa madeni ambayo nchi inaingia na kusababisha nchi wahisani
kuacha kuipa mikopo na kushindwa kujiendasha kwakua Tanzania inategemea bajeti
zake kutekelezwa kwa misaada.
Lakini pia
kumekuwepo na mashaka ya usalama wa nchi kutokana na majeshi yetu kujiendesha
kwa misaada na kisha kusababisha mpasuko kutokana na siasa zinazo enazoendelea
kama vile mgawanyiko wa muungano wetu,
Majadiliano hayo
yanafanyika nchi nzima kwa muda wa miezi miwili ijayo. Mpaka ifikapo Novemba
2014 muhtasar wa majadiliano utaandaliwa na kuchapwa katika machapisho ambayo
yatapelekwa kwa wadau wote ili kuongeza na kua na ushiriki mpana hasa ni kutia
chachu ya kitaifa na kua na ushiriki shadidi na ushahidi wa kutosha ili kusonga
mbele.























0 comments:
Post a Comment