Pages

Ads 468x60px

Monday, February 23, 2015

TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI

RAIS KIKWETE ATEUA WAKUU WA WILAYA WAPYA 27


*Atengua uteuzi wa Ma-DC 12, awabadilisha vituo 64, awabakiza 42 kwenye vituo vyao vya zamani

RAIS Jakaya Kikwete amefanya mabadiliko ya Wakuu wa Wilaya kwa kuwateua Wakuu wapya 27, kuwahamisha vituo vya kazi 64 na wengine 42 amewabakisha kwenye vituo vyao vya kazi vya zamani.

Akizungumza na waandishi wa habari kwenye ukumbi wa OWM TAMISEMI leo mchana (Jumatano, Februari 18, 2015) Waziri Mkuu Mizengo Pinda amesema mabadiliko hayo yamesababishwa na kuwepo kwa nafasi wazi 27 ambazo zilitokana na wakuu wa wilaya watatu kufariki dunia; kupandishwa cheo wakuu wa wilaya watano, kupangiwa majukumu mengine wakuu wa wilaya saba na kutenguliwa kwa uteuzi wa wakuu wa wilaya 12.

Hata hivyo, Waziri Mkuu alisema, Rais Kikwete amewabadilisha vituo vya kazi wakuu wa wilaya 64 na kuwabakiza kwenye vituo vyao vya zamani wakuu wa wilaya 42.

Wakuu wa Wilaya wapya 27 walioteuliwa ni Mariam Ramadhani Mtima anayeenda Ruangwa; Dk. Jasmine B. Tiisike anayeenda Mpwapwa; Pololeti Mgema (Nachingwea); Fadhili Nkurlu anayeenda Misenyi; Felix Jackson Lyaniva anayeenda Rorya na Fredrick Wilfred Mwakalebela anayeenda wilayaya Wanging’ombe.

Wengine na vituo vyao kwenye mabano ni Zainab Rajab Mbussi (Rungwe); Francis K. Mwonga (Bahi); Kanali Kimiang’ombe Samwel Nzoka (Kiteto), Husna Rajab Msangi (Handeni), Emmanuel J. Uhaula (Tandahimba); Mboni Mhita (Mufindi); Hashim S. Mgandilwa (Ngorongoro); Mariam M. Juma (Lushoto); Thea Medard Ntara (Kyela); Ahmad H. Nammohe (Mbozi); Shaban Kissu (Kondoa) na Stephen Zelothe (Musoma).

Wengine ni Pili Moshi (Kwimba); Mahmoud A. Kambona (Simanjiro); Glorius B. Luoga (Tarime); Zainab R. Telack (Sengerema); Bernard Nduta (Masasi); Zuhura Mustafa Ally (Uyui); Paulo Makonda (Kinondoni); Mwajuma Nyiruka (Misungwi) na na Maftah Ally Mohamed (Serengeti).

Wakuu wa Wilaya saba ambao uteuzi wao umetenguliwa lakini watapangiwa kazi nyingine ni Brig. Jenerali Cosmas Kayombo aliyekuwa Simanjiro; Kanali Ngemela E. Lubinga (aliyekuwa Mlele); Juma S. Madaha (aliyekuwa Ludewa); Mercy E. Silla (aliyekuwa Mkuranga); Ahmed R. Kipozi (aliyekuwa Bagamoyo); Mrisho Gambo (aliyekuwa Korogwe) na Elinas A. Pallangyo (aliyekuwa Rombo).

Waziri Mkuu pia aliwataja Wakuu wa Wilaya 12 ambao uteuzi wao umetenguliwa kutokana na sababu za umri, kiafya na kuimarisha utendaji Serikaini na wilaya zao kwenye mabano kuwa ni James K. Ole Millya (Longido); Elias Wawa Lali (Ngorongoro); Alfred Ernest Msovella (Kongwa); Danhi Beatus Makanga (Kasulu); Fatma Losindilo Kimario (Kisarawe); Elibariki E. Kingu (Igunga); Dk. Leticia Moses Warioba (Iringa); Evarista N. Kalalu (Mufindi); Abihudi M. Saideya (Momba); Martha J. Umbulla (Kiteto); Khalid J. Mandia (Babati) na Elias Goroi (Rorya).

(mwisho)

IMETOLEWA NA:

OFISI YA WAZIRI MKUU,




Wednesday, February 18, 2015

Kuingia kwa sekta ya afya katika BRN kunaleta matumaini mapya


Mtendaji mkuu wa Ofisi ya Rais, usimamizi wa utekelezaji wamiradi (PDB) Bwana Omari Issa, leo amekabidhi rasmi taarifa ya mkakati wa kuboresha sektaya afya chini ya BRN kwajumuia ya wahisani wa maendeleo. Makabidhiano hayo yamefanyika katika ofisi za PDB ambapo jumuiya yawahisani ilipatafursa ya kusikiliza kwa kina namna BRN inavyofanya kazi yakuleta matumaini mapya kwa watanzania kupitia sekta za kipaumbele.

Sekta ya afyaimekuwa ikijaribukuboresha utendaji wake lakini kuingia katika BRN kutaleta tija Zaidi. BRN inaamini katika misingi mikuu ambayo ni kuweka vipaumbele, kuwa na adabu ya utekelezaji,uwajibikaji
 na uaminifu, ufuatiliaji wa kina na wamara kwa mara na Mawasiliano thabiti kati ya watoa huduma nawapokea huduma. Hizi ni  nguzo muhimu zitakazo  tufikisha katika dira ya maendeleo ya taifa ya Mwaka 2025.

Awamu ya kwanza ya BRN iliziangazia sekta sita ambazo ni Kilimo, Elimu, Maji, Uchukuzi, Nishati na ukusanyaji wa mapato ambapo sekta za Afya na Uboreshaji wa mazingira ya Biashara zimeanza rasmi Mwaka huu. Sekta sitaza mwanzo zimedhihirisha mafanikio anuwai ambayo yaliwavutia jopo la wataalamu wamaendeleo wakiongozwa na Rais Mstaafu wa Botswana Bw Mogae. Ripoti kamili ya utekelezaji wa BRN kwa Mwaka wa kwanza itazinduliwa rasmi mape mamwezi Machi Mwaka huu.

Sekta ya afya inakusudia kutekeleza vipaumbele vine ambavyo ni mosi; ugawanyaji sawia wa wa huduma wa afya wenye ujuzi takikana kuanzia ngazi ya chini ya afya ya msingi, pili; utoaji huduma wenye ubora wa nyota tatu katika ngazi zote, tatu; upatikanaji wa dawa na bidhaa muhimu za afya katika ngazi zote, nne; kuimarisha afya ya uzazi nausalama wa mama na mtoto ilikupunguza vifo vya kundi hili muhimu kwa angalau asilimia 60ifikapo Mwaka 2018.

Jumuiya ya wahisani wamepongeza uamuzi wa kuiingiza sekta ya afya katika BRN na wa kithibisha utayari wao wakufanikisha mkakati huu, wametoa wito kwa wizara ya afya, PDB, Sekta binafsi na jamii ya kitanzania kwa ujumla kuhakikisha kuwa mkakati huu utafanikiwa.

Malengo haya yote yanahitaji juhudi kubwa na ya pamoja kutoka kwa jamii, wizara na taasisi zake zote hadi ngazi ya kijiji, wahisani wa maendeleo na sekta binafsi. “tusingoje nani aanze, sote tuwajibike, kila mmoja ajitazame kama anawajibika ipasavyo. Dira ya maendeleo ya Taifa tunayotaka  itupeleke kuwa nchi yenye uchumi wa kati haiwezi kufikiwa tusipofanya kazi kwa pamoja bila kunyoosheana vidole. BRN ni treni iliyoanza safari tayari, kila mmoja anawajibika kuingia kwa wakati na kwania Chanya, ukichelewa ukakuta imeondoka bado unafursa ya kuikimbilia kituo kinachofuata ilitwende pamoja” Bw Omari Issa ametoa wito huo kwa wahisani wa maendeleo najamii kwaujumla.

……………………………………………..xxxxxx………………………………………………..



Annastazia Rugaba, PDB habari, Februari 2015



Mtendaji Mkuuwa PDB Bw. Omari Issa akielezea umuhimu wa sekta ya Afya kuingia BRN kuungana na sekta nyingine zilizotangulia zinazoendelea kuzaa matunda

 

Bw. Omari Issa akimkabidhi mwakilishi wa wahisani wa maendeleo mkakati wa sektayaAfya chini ya BRN





Bw Issa na Dr. Sudha Sharma wa UNICEF Tanzania ambae ana wawakilisha jumuiya ya wahisani wa maendeleo baada ya makabidhiano








Mwakilishi wa jumuiya ya wahisani akipongeza uamuzi waserikari kuiweka sekta ya afya katika BRN



Naibu Katibu mkuu wa wizara ya afya Bw Michael akiwashukuru PDB kwaku simamia vizuri mchakato wa kuchagua vipaumbele vya sekta  yaafya chini ya BRN






Mmoja wa wahisani akisisitiza suala la uwajibikaji katika sekta ya afya





Bi. Sharon Crommer Mkuu wa USAID Tanzania akisisitiza ushiriki wa sekta Binafsi katika kuboresha Sekta ya afya Nchini Tanzania





Mmoja wa wahisani akisisitiza umuhimu wa wizara ya afya kuwajibika ki BRN katika maeneo mengine yasiyo ya kipaumbele katika BRN



Dr Oberline Kisanga wa kitengo cha mageuzi katika wizara ya afya akifafanua ushiriki wa TAMISEMI katika mkakati huuwa afya chini ya BRN



Bw Mugisha na Dr Linda wa PDB wakifurahia sehemu ya makabidhiano ya mkakati wa afya chini ya BRN

 

Sehemu ya washiriki watukio hili wakiwa katika ukumbi wamkutano wa  PDB