Pages

Ads 468x60px

Saturday, May 2, 2015

Kandoro awataka wananchi kujitokeza kwa wingi kujiandikisha katika daftari la kudumu.



Mkuu wa mkoa wa Mbeya Abass kandoro  amewataka wananchi kujitokeza kwa wingi kujiandikisha  kwenye dafutali la kudumu  la mpiga kura kwani  Vitambulisho vya  awali  havitumika kupiga kura  kwenye uchaguzi unatarajiwa kufanyika  octoba mwaka huu
Abass kandoro

Kandoro amesema hayo katika maadhimisho ya sikuuu ya wafanyakazi iliyofanyika katika uwanja wa kumbukumbu wa hayati sokoine jijini hapa  amewataka  wananchi kujitokeza kwa wingi katika kujiandikisha katika dafaftali la kudumu la mpiga kura utakapo fika ili kupati haki na sifa ya kupiga kura katika uchaguzi mkuu unaotarajia kufanyika October mwaka huu.

“Ninatoa wito kwa wafanyakazi wote na wananchi waliofikisha umri wa kupiga kura wajitokeze kwa wingi kujiandikisha katika daftali la kudumu la mpiga kura  ili upate haki ya kupiga kura ya kumpata Diwani, Mbunge hatimae Raisi unaemtaka, na lazima ujiandikishe kwani uchaguzi ujao utatumia vitambulisho vipya vile vya zamani havitatumika” amesema Kandoro

Ameongeza kuwa wananchi wanatakiwa  kutunza amani katika mchakato wote unaopelekea uchaguzi ili upite salama na kuvuka tukiwa salama bila kuingia katika machafuko na vita vitakavyo sababisha kushindwa kufanya shughuli za maendeleo ya wananchi na taifa kwa ujumla.

Aidha kandoro amesema  wananchi kwa kushirikiana na wafanyakazi  kwa pamoja wapige vita udini ukabila kwani ni moja ya sababu  zinzopelekea machafuko mahali popote duniani.
Tabia Mwanjotile

Akisoma Risala kwa mgeni Rasmi Tabia Mwanjotile  ameiomba Serikali kutazama upya ukusanyaji kodi kwa wafanya kazi kwakuwa umekuwa ni mzigo mkubwa ikiwepo makato mbalimbil ya mifuko ya kijamii na mikopo  na hivyo kuwafanya  waishi mazingira magumu na kushindwa kumudu gharama za kuendesha maisha .

Akizungumzia swala  upandaji wa bidhaa mbalimbali ikiwemo umeme,majina na ges   mwanjotile  amesema vimekuwa vikipanada  kila mara bila  kuangalia  kipato cha  mfanyakazi  wa kima cha chini  na hivyo  kuendelea kumdidimiza mfanyakazi.

 Zegge Pilipili mwaenyekiti TUCTA Mkoa wa Mbeya akimkaribisha mgeni Rasmi uhutubia Wafanyakazi


                                                         Viongozi mbalimbali wa TUCTA
Mwanafunzi wa Chuo kikuu Teku Aliejiite kwa jina la madodoso akiongea utenzi wenye ujumbe wa siku ya wafanyakazi.


                                                         Kundi la Lizombe likitoa burudan







                                   Baadhi ya viongozi na wafanyakazi walifika katika madhisho


         Waandishi wa habari kutoka vyombo mbalimbali wakiendelea na majukumu ya kihabari





























Taasisi na makampuni mbalimbali yalpata fulsa ya kuonesha shughuli zao mbele ya mgeni Rasmi

0 comments:

Post a Comment