ZAIDI YA ALAMA
40 ZA KUONGOZEA MAGARI BARABARA YA CHUNYA MBEYA ZIMEIBWA
Katika hari
isiyo ya kawaida watu wasiojulikana wameyaondoa mabomba yenye alama zakuongozea
magari katika barabara mpya itokayo Mbeya kwenda Chunya,
Hali hiyo
imejitokeza wakati zimebakia siku chache za kukamilika kwa mradi huo na
kuukabidhi kwa mwajiri ambae ni TANROAD
Akizungumza kwa masikitiko makubwa Eng: Paul Lyakurwa
meneja wa Tanroad mkoa wa mbeya katika mkutano wa hadhara na wananchi waishio
karibu na mradi huo amesema ni vitendo vya aibu na visivyo vumilika na kwamba
waliohusika lazima wanafahamika kwakuwa sehemu zilizo ondolewa vyuma hivyo ni
makazi ya watu hivyo si rahisi
kutowafahamu.
Naye mgeni
rasmi wa mkutano huo Nyerembe Munasa mkuu wa wilaya ya Mbeya amewataka wenye
viti wa serikal za mitaa kufanya uchunguzi kwa kushirikiana na jeshi la polisi
ili kuwabaini waliofanya vitendo hivyo haraka iwezekanvyo na kuwachukulia hatua
stahiki.
Mmoja wa
wananchi waishio kando ya maradi huo Jamesi kilumbo amesema baadhi ya sababu
zinazopelekea vijana kuziondoa alama hizo ni ugumu wa maisha na ukosefu wa
ajira hivyo kukosa pesa za kujikimu pamoja na vitendo vya uvutaji bangi na ulevi
wa kupindukia.
Pia Helena
mwanjabili makazi wa Isanga imeitaka mamlaka husika kutoa elimu ya kutosha
kuhusu umuhimu wa alama hizo kwa wananchi waishio pembezoni mwa barabara hiyo
na kwamba kila mmoja awe na jukumu la kuona linamhusu kulinda ili vitendo hivyo
viijirudii tena.
MWISHO
0 comments:
Post a Comment