Na Magreth Kinabo-MAELEZO
Askofu Mkuu wa Jimbo Kuu la Katoliki la Dar es salaam,Muadhama, Kardinali Pengo
amesema kwamba ameridhishwa na huduma za afya zinazotolewa katika
Hospitali ya Taifa ya Muhimbili(MNH), hivyo itakuwa ni vigumu kwa
Serikali kumshawishi kwenda kutibiwa nje ya nchi.
Kauli leo na Askofu Pengo ambaye amelezwa katika Taasisi ya Moyo ya Jakaya Kikwete iliyopo katika hospitali ya MNH jiji Dar es Salaam kuanzia Januari Mosi, mwaka 2016 hadi sasa mara baada ya kuzungumza na Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Ummy Mwalimu ambaye alimtembelea leo mchana ili kuweza kufahamu maendeleo ya afya yake.
“Ninapenda kutoa taarifa kwa umma wa Watanzania na kuwaondoa hofu kuwa hali ya Baba Askofu Pengo imeimarika na anaendelea vizuri, hajawekewa oxygen wala hajalazwa katika wodi ya uangalizi maalum(ICU) na ameridhika na huduma zinazotolewa.
“Ameridhika na huduma zinazotolewa za moyo, itakuwa ni vigumu sisi kama Serikali kumshawishi kwenda kutibiwa nje ya nchi, ” alisema Waziri huyo.
Aidha Waziri Ummy
alitembelea sehemu ya ICU, katika taasisi hiyo, ambapo alisema
operesheni ambazo ni ngumu zinafanyika, katika opresheni za moyo kiwango
cha kimataifa ni asilimia 6, wakati Tanzania imefikia kiwango cha
asilimia 4, hivyo tunafanya vizuri.
Aliongeza kwamba
hatua hiyo inapunguza idadi ya wagonjwa wanaokwenda kutibiwa nje ya
nchi, pia aliwataka hata wagonjwa kutoka taasisi binafsi kwenda kutibiwa
katika taasisi hiyo.
Kwa upande wake Mkuu wa taasisi hiyo, Profesa Mohamed Janabi alisema Baba
Askofu huyo ameridhika na matibabu aliyoyapata ambayo yanaweza
kufanyika Tanzania, hivyo changamoto iliyopo kwa Serikali kupitia wizara
hiyo ni kuiwezesha taasisi hiyo kibajeti ili kuwezesha wagonjwa
anagalau 50 kati ya 300 ambao wako kwenye orodha ya kupatiwa huduma.
Aliongeza kwamba Baba Askofu huyo, ataruhusiwa siku za karibuni, baada ya hali kuendelea vizuri.
0 comments:
Post a Comment