Pages

Ads 468x60px

Wednesday, January 13, 2016

Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo akutana na Bodi ya Wakurugenzi ya TBC

9689-mkurugenzi mshana
Mkurugenzi Mtendaji wa TBC, Clement Mshana ambaye pia ni Katibu wa bodi ya wakurugenzi ya TBC akimueleza jambo Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Mh. Nape Nnauye leo jijini Dar es Salaam walipokutana kuzungumzia changamoto mbali mbali za Shirika hilo.
9705-tbc bodi
Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Mh. Nape Nnauye akiongea na wajumbe wa Bodi ya wakurugenzi ya Shirika la Utangazaji Tanzania (TBC) leo hii jijini Dar es Salaam. Mhe. Nape alifanya kikao na Bodi hiyo ili kuzungumzia changamoto mbalimbali zinazolikabili shirika hilo na jinsi ya kuyapatia ufumbuzi.Kulia kwa waziri ni Mwenyekiti wa Bodi hiyo Bi.Mwajabu Possi.
9692-wajumbe wa bodi
Baadhi ya wajumbe wa Bodi ya wakurugenzi ya Shirika la Utangazaji Tanzania (TBC) wakimskiliza Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Mh. Nape Nnauye (hayupo pichani)  jijini Dar es Salaam.

0 comments:

Post a Comment