JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA
TAASISI YA KUZUIA NA KUPAMBANA NA RUSHWA
Mkuu wa TAKUKURU (M) Ilala,
S.L.P 6420, Kinondoni
Simu : (022)2861088 Nukushi 2150047
Barua pepe: rbcilala@pccb.go.tz
Wavuti www.pccb.go.tz
Ofisi ya TAKUKURU Mkoa wa Ilala imemkamata afisa wa ofisi ya
uhamiaji Mkoa wa Dar es Salaam kwa tuhuma ya kuomba shilingi milioni 1
na kupokea Shilingi laki 5 kutoka kwa mfanyabiashara mwenye asili ya
Kisomali mnamo tarehe 4 Februari, 2016.
Bw.Kiangwike Ngumba mwenye cheo cha afisa mkaguzi wa uhamiaji
alikamatwa baada TAKUKURU kupokea taarifa kutoka kwa Bw.Bille Mohamed
kuwa mtuhumiwa na maafisa wengine walifika katika eneo lake la biashara
na kuchukua hati ya kusafiria ya ndugu yake kwa madai kuwa wanakwenda
kuifanyia ukaguzi. Hata hivyo, baadaye afisa huyo alimtaka mtoa taarifa
kutoa kiasi cha shilingi milioni moja kama sharti la kurejesha hati
hiyo.
Uchunguzi wa tuhuma hii unaendelea ikiwa ni pamoja na kuwafuatilia
na kuwachunguza maafisa wengine waliohusika ili wafikishwe mahakamani.
Afisa huyo na wenzake wanakabiliwa na tuhuma ya kuomba na kupokea rushwa
kinyume na kifungu cha 15 cha Sheria ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa
Na.11 ya mwaka 2007.
Tunatoa wito kwa wananchi kuendelea kujitokeza kuripoti vitendo au
viashiria vyovyote vya rushwa dhidi ya watumishi wasio waadilifu katika
ofisi za TAKUKURU ili hatua za kisheria zichukuliwe dhidi yao.
IMETOLEWA NA RAPHAEL MBWAMBO- MKUU WA TAKUKURU MKOA WA ILALA 05/2/2016
0 comments:
Post a Comment