Waziri wa Viwanda,Biashara na Uwekezaji Mhe. Charles John
Mwijage akijibu hija mbalimbali toka kwa wabunge katika kikao cha 9 cha
Bunge la 11 linaloendelea Mjini Dodoma Picha na Raymond Mushumbuai
MAELEZO
(Na Raymond Mushumbusi-MAELEZO)
Shillingi
Billioni 60 zinategemea kutumika kufufua kiwanda ya matairi cha General
Tyres kilichopo Jijini Arusha ambacho kimesharudi mikononi mwa Serikali,
na fedha hizo zitatumila kurekebisha mitambo ya umeme ya kiwanda hicho
na kupata mitambo mipya itakayoendana na teknolojia ya utengenezaji wa
matairi duniani.
Akijibu swali la
Mhe. Joshua Nassari Mbunge wa Arumeru Mashariki (CHADEMA) lililouliza ni
lini serikali itafufua kiwanda cha matairi cha General Tyres kilichopo
Jijini Arusha kwani ni tegemeo kwa ajira kwa wananchi wa Jijini la
Arusha,Waziri wa Viwanda,Biashara na Uwekezaji Mhe.Charles John Mwijage
amesema kiwanda hicho kimesharudi mikononi mwa Serikali na wako mbioni
kukifufua ili kianze kufanya kazi ya kuzalisha matairi nchini.
“
Tumeanzisha viwanda nchi ili kuzalisha bidhaa na kutoa ajira kwa
watanzania na sio kuwatesa wananchi kwa kukosa ajira au kuagiza bidhaa
ambazo tunaweza kuzalisha hapa hapa nchini, hivyo basi Serikali kupitia
Wizara yangu tutatenga fedha kwa ajili ya kufufua kiwanda hiki ili
kianze kufanya kazi mara moja”
“
Sio tu tutafufua kiwanda cha General Tyres pekee bali tunafatilia
viwanda vyote ambavyo vimekiuka sheria na kanuni kwa kutoviendeleza
viwanda hivyo ili kuvirudisha mikononi mwa Serikali au kuwatafuta
wawekezaji wengine watakaoweza kuviendesha viwanda hivyo” Alisema Mhe.
Mwijage.
Aidha Mhe. Charles John
Mwijage amesema ni kweli makampuni mengi yaliyobinafsishwa hayakufanya
vizuri katika uendeshaji wake ukiacha mifano ya makampuni machache
yanayofanya vizuri yakiwemo Tanzania Breweries Limited (TBL),Morogoro
Polyester 21st Century na Tanzania Cigarette Company Limited
(TCC), hivyo Wizara yangu ikishirikiana na Msajili wa Hazina juu ya
Viwanda ilifanya tathmini iliyoonesha kuwa mashirika mengi
yaliyobinafsishwa hawakutekeleza mikataba ya mauziano kikamilifu.
Ameongeza
kuwa lengo ni kuhakikisha makampuni yote haya yanazalisha kwa tija ili
tupate bidhaa,kodi ya Serikali na ajira kwa wananchi wa Tanzania ili
kutimiza adhma ya Mhe.Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe.John
Pombe Joseph Magufuli ya kuwa na Tanzania yenye viwanda kwa maendeleo ya
taifa.
Serikali kupitia
Wizara yetu inaboresha mazingira ya uwekezaji hali itakayowajengea imani
kwa wawekezaji na kupelekea kupanua zaidi shughuli zao za kibiashara na
pia kuendeleza mpango wa Viwanda vidogo na vya kati unaoshirikisha SIDO
na Halmashauri za Wilaya na Mikoa ili kuanzisha Viwanda vya Mkoa vya
kuongeza thamani ya bidhaa za Kilimo,Uvuvi na ufugaji kupitia njia hii
ajira nyingi zitaongezeka na kupunguza tatizo la ajira nchini.
0 comments:
Post a Comment