Na. Lilian Lundo - Maelezo
Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora Mhe. Angellah  Kairuki amemsimamisha  kazi aliyekuwa mkuu wa chuo cha Utumishi wa Umma Said Nassoro kutokana na kushindwa kusimamia watumishi walioko chini yake
Mhe. Kairuki ametoa maamuzi hayo leo jijini Dar es Salaam  katika mkutano na waandishi  wa  habari katika moja ya kumbi zilizopo katika ofisi za Utumishi wa Umma.
“Namsimamisha Bwana Said Nassoro aliyekuwa mkuu wa chuo hiki kwa kushindwa kusimamia watumishi walioko chini yake  na
 kupelekea suala zima la usimamizi wa shughuli za chuo hususani katika 
matawi yake mbalimbali yaliyoko mikoani kuathirika,” alisema Mhe. 
Kairuku.
Mhe. Kairuki aliongeza kwa kusema kuwa usimamizi  wa Bw. Nassoro  ambao haukuwa wa ufanisi umetoa mwanya kwa viongozi mbalimbali wa matawi kufanya ubadhilifu wa mali za Umma ambapo mwaka  2011 na 2013 aliyekuwa mkurugenzi wa chuo upande wa tawi la Mtwara Silvanus Ngata aliongeza gharama za ujenzi.
Aidha
 taarifa kutoka Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG) pamoja na 
TAKUKURU zilithibitisha ubadhilifu huo lakini mkuu huyo wa chuo hakuweza
 kuchukua hatua yoyote badala yake alimuhamisha Bw. Ngata kwenda kwenye 
tawi la Tabora na kuendelea na wadhifa wake. 
Kutokana na ubadhilifu huo imempelekea Mhe. Kairuki  kumsimamisha
 kazi Bw. Ngata ambaye alikuwa Mkurugenzi wa Chuo cha Utumishi wa Umma 
tawi la Tabora na Bw. Joseph Mbwiro kutokana na matumizi mabaya ya fedha
 za malipo ya ada kiasi cha shilingi bilioni moja ambazo zilikuwa 
zikilipwa na wanafunzi kwa mwaka wa fedha 2014/15.
Mhe. Kairuki ameendelea kueleza kuwa  bado wanaendelea kuondoa watumishi wa Umma ambao hawafuati   mifumo na miongozo ya Utumishi wa Umma ili kuwabakiza  watumishi ambao wanaonyeshe taswira nzuri na kufuata mifumo na  miongozo  ya Utumishi wa Umma kwa ukamilifu wake.

0 comments:
Post a Comment