Bw Polepole akizungumza leo katika kongamano la shirikisho la wanafunzi wa Vyuo vya juu Iringa , shirikisho la CCM
Polepole akisalimiana na Diwani wa kata ya Nduli Bw Bashir Mtove
Mkuu wa Wilaya ya Iringa Bw Richard Kasesela kushoto akiwa na Kamanda wa Uvccm Mkoa wa Iringa Bw Salim Asas
Na Matukiodaimablog
MWANAHAKATI Humphrey Polepole amesema chama cha mapinduzi ( CCM) ni chama Chenye misingi ya kweli ya kuwatumikia wananchi ukilinganisha na vyama vingine asema Kazi ya kutumbua majipu ni nzuri
Huku akiwataka wana CCM jimbo la Iringa Mjini kuanza Kazi ya kueleza mambo mazuri yanayofanywa na Rais Dr John Magufuli katika utekelezaji wa Ilani ya CCM.
Kuwa jimbo la Iringa halikuwa la kwenda mikononi mwa upinzani ataka viongozi wa CCM kujitathimini na kuona wapi walipoanguka.
Akizungumza wakati wa ufunguzi wa kongamano la shirikisho la Vyuo vya elimu ya juu la CCM Mkoa wa Iringa Bw Polepole alisema kuwa utendaji mzuri wa serikali ya Dr Magufuli katika kutekeleza Ilani ya CCM umedhihirisha wazi aina ya wana CCM ambao ni hazina na wanaweza kuleta maendeleo makubwa katika jamii
Kwani alisema kinachofanywa na Rais Dr Magufuli katika kuwatumikia watanzania ni wazi kila Mwananchi anatambua sasa hazina kubwa iliyopo ndani ya chama kwa kutokana na mazuri ambayo Serikali inafanya kazi.
Bw Polepole alisema kuwa ni kweli CCM imepata ushindi katika uchaguzi mkuu uliompa nafasi ya kwenda Ikulu Rais Dr Mahufuli japo alisema ushindi huo wa asilimia 58 bado si mzuri wa kujivunia na kutaka nguvu iongezwe zaidi ili kurudi katika ushindi wa asilimia 80 hadi 88
Alisema kuwa njia pekee ya kuongeza ushindi wa CCM ni lazima kufanya Kazi kukijenga chama na Kazi zake.






0 comments:
Post a Comment