JENGO LA KIWANDA CHA HISOOP LIMEGEUZWA KUA MAKAZI YA POPO
Chama cha waandishi wa uwekezaji na utalii Tanzania (TAJATI)
watembelea kiwanda cha Sabuni cha hisop kilichopo iyunga jijini Mbeya na
kujionea jinsi kilivyo filisiwa na wawekezaji wasio kua na huruma kwa nchi hii
kwa kuiuwa kiochumi.
Waandishi hao wameshuhudi mazingira ya kiwanda hicho
kugeuzwa kua mashmba ya maharagwe na mahindi badla ya utengenezaji wa sabuni
iliyokua ikipendwa na wananchi wa mkoa huu, lakini pia kiwanda hicho kilitoa
ajira kwa vijana.
Cha kushangaza sana katika kiwanda hicho hakuna kinacho endelea,
isipokua ndani ya godauni hilo waandishi
wameshuhudi kung`olewa kwa vipuli vyote vya mashine na kuliacha gofu lililopo kua
makazi ya popo baada ya kuliacha kwa muda mlefu bila kazi yoyote.
Akiongea mmoja wa walinzi waliopo hapo ambae hakutaka jina
lake litajwe amesema hajawahi kuona jingo hilo likifunguliwa kwa muda mlefu
sana na hamjui hata mmiliki wa eneo hilo tangu apangwe na viongozi wa kampuni
yake kulinda lindo hilo amekua akifika na kuondoka bila kuona kitu chochote
kinachoendelea.
Makamu mwenyekiti wa TAJATI ametoa wito kwa mamlaka husika
kutupia jicho la pekee kwa wawekezaji wenye lengo baya la kuhujumu uchumi wa nchi
kwa viwanda hivi ambavyo vilitoa manufaa kwa wananchi na taifa kwa ujumla.
WAANDISHI WAKIONGE NA MLINZI WALIPOWASILI KATIKA KIWANDA HICHO
![]() |
WAANDISHI WALIPATA NAFASI YA KUTEMBE NDANI YA KIWANDA HICHO |
![]() |
MAKAMU MWENYEKITI CHRISTOPHA NYENYEMBE AKISHANGA KUHALIBIWA KWA MIUNDO MBINU |
![]() |
ILICHO IBAINI KAMRA YA MWANDISHI NGULI RASHID MKWINDA KUPITIA UPENYO HUU KILICHOPO NDANI YA KIWANDA HIKI |
WAANDISHI WAKITOA MAONI JUU YA WALICHO KIONA KWA VYOMBO VYA HABARI
0 comments:
Post a Comment