Aibu zake
zamefanya awe na thamani, Waandishi wa Habari za Utalii na uwekezaji Tanzani
(TAJATI) wa msaka kwa udi na uvumba ili kumshuhudia.
Nyani Kipunji
Hifadhi ya Mazingira ya Asili ya milima ya
Rungwe Ni hifadhi inayo patikana Wilaya ya Rungwe mkoani mbeya,Iili hifadhiwa
mwaka 1949 kwa lengo la kuhifadhi vyanzo vya maji na baionuai Hifadhi hii
inaumbali wa km 25 kusini mashariki mwa
mji wa Mbeya na km 7 kusini mwa mji wa Tukuyu.
Baada ya kuona umuhimu wa hifadhi ya Mlima
Rungwe, mchakato wa kupandisha hadhi ulianzishwa mwaka 2008 na hatimaye mwaka
2009 hifadhi ilipandishwa hadhi na kuwa Hifadhi ya Mazingira Asilia. Hifadhi ya
Mazingira Asilia ni hadhi ya juu kuliko Msitu wa Hifadhi. Hifadhi ya Mazingira
Asilia hairuhusu matumizi mengine zaidi ya elimu, utafiti na utalii.
Kutokana na sifa za
kipekee za Hifadhi ya Mazingira Asilia
ya Mlima Rungwe: ikiwemo urefu wa mlima, mashimo ya volukano (paluvalutali,
Lusiba na Ng’ombe) na wanyama aina ya kipunji, na maji moto. Vyote hivi
vimekuwa vinashawishi watalii kutembelea hifadhi yenye mazingira asilia ya mlima Rungwe. Pia hifadhi
imepakana na hifadhi ya Kitulo ambayo ina vivutio vingi vya kitalii.
Hayo ndiyo yamepelekea kua
kishawishi kikubwa kwa waandishi wa Habari za Utalii na uwekezaji Tanzania (TAJATI)
kutembelea na kupanda mlima huo ili kujionea mambo hayo akiwepo Nyani aina ya
kipunji mwenye sifa moja kubwa ya aibu ambayo inamfanya asionekene kwa urahisi
kwa watu.
Akionge na waandishi wa
habari mhifadhi mkuu wa mlima Rungwe Inocent Lipembembe amesema Nyani aina ya
Kipunji haonekani kirahisi kutokana na aibu alizo nazo kwani hapendi kuonekana kilahisi
kwa watu
“Pamoja na yote yaliyo
kivutio kwa watalii katika mlima huu
yupo nyani Kipunji ambae hapatika ulimwenguni kote isipokua katika mlima Rungwe
na ndiye kivutio kwa watalii na unapotaka kumuona lazima utoe taalifa mapema
ili kuwaandaa watu maalumu ili kumtafuta mapema na ndipo wale waonataka kumuona
tunawasiliana nao” Amesema Lupembe
Ameongeza kua Kutokana na sifa za kipekee za Hifadhi ya Mazingira Asilia ya Mlima Rungwe: ikiwemo
urefu wa mlima, mashimo ya volukano (paluvalutali, Lusiba na Ng’ombe) na maji moto. Vyote hivi vimekuwa vinashawishi
watalii kutembelea hifadhi yetu ya mazingira asilia ya mlima Rungwe. Pia
hifadhi imepakana na hifadhi ya Kitulo ambayo ina vivutio vingi vya kitalii.
Mwandishi wa habari wa Blog hii Charles Abraham
Waandishi kufika getini kabla ya kuingia Hifadhini Kulia ni makamu mwenyekiti wa (TAJATI) Christopha Nyenyembe na Ezekiel Kamanga
Mhifadhi mkuu Inocent Lipembembe akiongea jambo kwa waandishi wa habari kabla ya kupanda mlima
Mwandishi wa habari Rashid Mkwinda akifuatilia kwa makini jambo
Waandishi wakipanda Mlima Rungwe



















0 comments:
Post a Comment