Pages

Ads 468x60px

Thursday, April 28, 2016

Rais Dkt JOHN MAGUFULI awaapisha Makatibu Tawala Wapya 10

Na Mwandishi Maalum, Ikulu

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli amewaapisha Makatibu Tawala wapya kumi aliowateua tarehe 25 Aprili, 2016 na kuwapangia vituo vyao vya kazi.

Makatibu Tawala hao wameapishwa leo tarehe 27 Aprili, 2016 Ikulu Jijini Dar es salaam na kisha wametia saini hati ya ahadi ya uadilifu kwa viongozi wa umma, zoezi lililoendeshwa na Kamishna wa maadili Sekreatieti ya Maadili ya Viongozi wa Umma, Mheshimiwa Jaji Salome Kaganda na kushuhudiwa na Katibu Mkuu Kiongozi Balozi John Kijazi.

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akimuapisha Ndugu Jumanne Abdallah Sagini kuwa Katibu Tawala wa Mkoa wa Simiyu, Ikulu jijini Dar es Salaam.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akimuapisha Ndugu Selestine Muhochi Gesimba kuwa Katibu Tawala wa Mkoa wa Geita, Ikulu jijini Dar es Salaam.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akimuapisha Eng. Aisha Salim Amour kuwa Katibu Tawala wa mkoa wa Kilimanjaro, Ikulu jijini Dar es Salaam.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akimuapisha Eng. Zena Ahmed Said kuwa Katibu Tawala wa mkoa  wa Tanga, Ikulu jijini Dar es Salaam.

Makatibu Tawala walioapishwa ni;

1.      Arusha -          Richard Kwitega
2.      Geita -             Selestine Muhochi Gesimba
3.      Kagera -          Armatus C. Msole
4.      Kilimanjaro -  Eng. Aisha Amour
5.      Pwani -            Zuberi Mhina Samataba
6.      Shinyanga -     Albert Gabriel Msovela
7.      Singida -          Dr. Angelina Mageni Lutambi
8.      Simiyu -          Jumanne Abdallah Sagini
9.      Tabora -          Dkt. Thea Medard Ntara
10.  Tanga -            Eng. Zena Said

Makatibu Tawala wengine wa Mikoa ambao hawakuapishwa leo, ni wale waliohamishwa vituo vya kazi na wale waliobaki katika vituo vya kazi walivyokuwepo, ambao tayari walishakula kiapo cha kuwa Katibu Tawala wa Mkoa.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiwa katika picha ya pamoja na Makatibu Tawala wapya wa Mikoa 10 mara baada ya Kuwaapisha, Kulia kwake. 
Rais Dkt. John Pombe Magufuli akijadiliana jambo na Makamu wa Rais Samia Suluhu Hassan pamoja na Katibu Mkuu Kiongozi Balozi Eng. John Kijazi mara baada ya kumaliza kuwaapisha Makatibu Tawala wa mikoa 10 Ikulu jijini Dar es Salaam. 

PICHA NA IKULU

0 comments:

Post a Comment