Kwa mara
nyingine tena Tanzania inashiriki katika onesho la kimataifa la Utalii
la INDABA yanayofanyika huko Afrika Kusini maonesho hayo yalianza jana
tarehe 7 Mei na yanatarajiwa kumalizika tarehe 9 Mei, 2016. jijini
Durdan, Bodi ya Utalii (TTB) ndio waratibu wa onesho kwa upande wa
Tanzania. Katika onesho hili TTB inashirki pamoja na taasisi za TANAPA
na Mamlaka na Hifadhi ya Ngorongoro pamoja na makampuni mbalimbali
binafsi Zaidi ya 30 ya sekta ya Utalii .
Katika
siku yake ya kwanza Banda la Tanzania limetembelewa na wadau wengi
wakiwemo watalii, waandishi wa habari za utalii, mawakala wa Utalii nk.
Miongoni mwa watu mashuhuri waliotembelea Banda la Tanzania ni Mwandishi
maarufu na mtangazaji wa Kimataifa kutoka Shirika la habari la CNN la
Marekani Bwana Richard Quest ambaye alifurahishwa na vivutio vua utalii
nchini Tanzania mara baada ya kupata maelezo kutoka kwa Maofisa wa Bodi
ya Utalii Tanzania TTB.
Mkurugenzi
wa Masoko kutoka Bodi ya Utalii Tanzania TTB Bwa Philip Sebastian
akimuonyesha jambo Mwandishi maarufu na mtangazaji wa Kimataifa kutoka
Shirika la habari la CNN la Marekani Bwana Richard Quest wakati
alipotembelea katika banda la Tanzania katika maonesho ya kimataifa ya
Utalii Indaba jijini Durban nchini Afrika Kusini..
Mkurugenzi
wa Masoko kutoka Bodi ya Utalii Tanzania TTB Bwa Philip Sebastian
akimpa maelezo kuhusu vivutio vya utalii nchini Tanzania Mwandishi
maarufu na mtangazaji wa Kimataifa kutoka Shirika la habari la CNN la
Marekani Bwana Richard Quest wakati alipotembelea katika banda la
Tanzania katika maonesho ya kimataifa ya Utalii Indaba jijini Durban
nchini Afrika Kusini Katikati ni Bi Devotha Mdachi Mkurugenzi wa Bodi ya
Utalii Tanzania TTB.
Baadhi
ya wagenimbalimbali waliotembelea katika banda la Tanzania katika
maonesho ya Utalii ya Indaba yanayofanyika katika jiji la Durban nchini
Afrika Kusini.
Mkurugenzi
wa Masoko kutoka Bodi ya Utalii Tanzania TTB Bwa Philip Sebastian na
Bi. Devotha Mdachi Mkurugenzi wa Bodi ya Utalii Tanzania TTB. wakiwa na
mmoja wa wageni aliyetembelea katika banda la Tanzania katika maonesho
ya kimataifa ya Utalii Indaba jijini Durban nchini Afrika Kusini.
Baadhi ya wageni wakipata taarifa mbalimbali kutoka katika banda la Tanzania.
0 comments:
Post a Comment