


………………
Serikali
imesitisha wimbo na Video ya Muziki wa Chura wa Msanii Snura Mushi
kuchezwa kwenye vyombo mbalimbali vya habari kuanzia leo mpaka pale
msanii huyo atakapoifanyia marekebisho video ya wimbo huo.
Usitishwaji huo umetokana na maudhui ya utengenezwaji wa Video hiyo ambayo haiendani na maadili ya Mtanzania.
Pia
Serikali imesitisha maonyesho yote ya hadhara ya mwanamziki huyo mpaka
pale atakapo kamilisha taratibu za usajili wa kazi zake za Sanaa katika
Baraza la Sanaa la Taifa (BASATA).
Serikali
inawataka wasanii kujiuliza mara mbili kabla ya kubuni kazi zao za
Sanaa. Wafikirie wazazi, ndugu, jamaa na marafiki zao watazipokeaje?
Wavae nafasi ya wale wanaowadhalilisha, Waelewe kwamba Sanaa si uwanja
wa kudhalilisha watu hata kidogo..
Aidha
Serikali imechukizwa na kazi hiyo ambayo si tu inadhalilisha tasnia ya
Muziki bali inadhalilisha utu wa mwanamke na inaifanya jamii kuanza
kuhoji hadhi ya msanii, weledi na taaluma ya Sanaa kwa ujumla.
Serikali
inawakumbusha wananchi wote kutokujiingiza katika makosa ya sheria ya
mtandao kwa kusambaza wimbo huu kwa njia yoyote ile ya kimtandao
Pia
inavitaka Vyombo vya habari viwe vya kwanza kuchuja maudhui ya kazi
yoyote ya Sanaa kabla ya kuwa mawakala wa uharibifu wa jamii kupitia
kucheza kazi chafu za Sanaa.
Serikali
inatoa wito kwa wasanii wote kuzingatia maadili ya Kitanzania kabla ya
kutoa kazi zao kwani haitawavumilia ‘wasanii’ wachache ambao wanataka
kuigeuza tasnia ya Sanaa kuwa sehemu ya uvunjifu wa maadili.
Imetolewa na Zawadi Msalla
Kaimu Mkuu wa Kitengo cha Mawasiliano Serikalini
0 comments:
Post a Comment