Uhusiano kati ya
Marekani na Tanzania unaonesha dalili za kuimarika licha ya nchi hiyo
kukatiza msaada wa awamu ya pili ya mradi wa changamoto za milenia
(MCC-2) kwa Tanzania.Balozi wa Marekani nchini Tanzania
Mheshimiwa Mark Childress amesema hayo baada ya kukutana na kufanya
mazungumzo na rais wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli.Bwana
Childress alisema kuwa hivi karibuni ''kupitia shirika la misaada la
Marekani, USAID tunatarajia kutia saini mkataba wa zaidi ya dola milioni
400 kwa ajili ya mwaka ujao.''Aidha tumezungumza kuwa kutakuwa
na dola milioni 800 zitakazotolewa na Marekani kwa ajili ya miradi
mbalimbali na hii haihusiani na MCC.'' Alisema balozi Childress"Ukweli ni kwamba tunayo mengi ya kufanya pamoja katika sekta mbalimbali
zikiwemo afya, elimu na kilimo na tutafanya kila juhudi kuhakikisha
yanafanikiwa"Rais Magufuli kwa upande wake alisema kuwa serikali yake itaendeleza kuimarisha zaidi uhusiano na ushirikiano na Marekani. Aidha rais huyo alisema kwamba fedha za msaada kutoka Marekani ni muhimu kwa maendeleo ya Tanzania."Amekuja
kutuhakikishia kwamba watatoa hela kwa ajili ya Tanzania na anasema
sasa hivi watatoa zaidi ya dola milioni 800, na mkataba mwingine
tunaweza tukasaini hata kesho wa dola milioni 410.Rais Magufuli
alisema ''Balozi anasema kutotoa hela za MCC hakuna maana kupotea kwa
urafiki wa Tanzania na Marekani, urafiki wa Tanzania na Marekani upo
pale pale na sasa wanaongeza hela nyingi zaidi katika kuonesha kwamba
juhudi za ''Hapa kazi tu'' zinaendelea" Taarifa hiyo ya ikulu ilielezea.
0 comments:
Post a Comment