Mgeni
rasmi katika hafla ya TAMWA wakizinduwa mradi wa kampeni ya kupambana
na ajali za vyombo vya moto barabarani, Kamanda wa Polisi wa Kikosi cha
Usalama Barabarani, Mohammed Mpinga akizungumza kabla ya kuzindua mradi
huo. TAMWA wamezindua mradi huo ikiwa ni jitihada za kupunguza ajali
hizo ambazo zimekuwa zikigharimu maisha ya wanawake, watoto pamoja na
jamii nzima.
Mkurugenzi
Mtendaji wa TAMWA, Bi. Edda Sanga (kushoto) akizungumza katika hafla ya
uzinduzi wa mradi wa kampeni ya kupambana na ajali za vyombo vya moto
barabarani ikiwa ni jitihada za kupunguza ajali hizo ambazo zimekuwa
zikigharimu maisha ya wanawake, watoto pamoja na jamii nzima.
Mkurugenzi
Mtendaji wa TAMWA, Bi. Edda Sanga akizungumza katika hafla ya uzinduzi
wa mradi wa kampeni ya kupambana na ajali za vyombo vya moto barabarani
ikiwa ni jitihada za kupunguza ajali hizo ambazo zimekuwa zikigharimu
maisha ya wanawake, watoto pamoja na jamii nzima.
Ofisa
Miradi Mkuu, TAMWA, Bi. Gradness Munuo (kulia) akitambulisha mradi huo
kwa washiriki wa hafla ya uzinduzi wa mradi wa kampeni ya kupambana na
ajali za vyombo vya moto barabarani.
Baadhi
ya maofisa kutoka TAMWA (wa kwanza na wa pili kulia) wakifuatilia
mijadala anuai pamoja na washiriki wengine katika hafla ya uzinduzi wa
mradi wa kampeni ya kupambana na ajali za vyombo vya moto barabarani.
Mkurugenzi
Mtendaji wa TAMWA, Bi. Edda Sanga (kushoto) akizungumza katika hafla ya
uzinduzi wa mradi wa kampeni ya kupambana na ajali za vyombo vya moto
barabarani ikiwa ni jitihada za kupunguza ajali hizo ambazo zimekuwa
zikigharimu maisha ya wanawake, watoto pamoja na jamii nzima.
Baadhi
ya washiriki wa hafla ya TAMWA wakizinduwa mradi wa kampeni ya
kupambana na ajali za vyombo vya moto barabarani wakifuatilia mada
mbalimbali zilizokuwa zikiwasilishwa na wadau anuai.

CHAMA cha Wanahabari Wanawake
Tanzania (TAMWA) kimezindua mradi wa kampeni ya kupambana na ajali za
vyombo vya moto barabarani ikiwa ni jitihada za kupunguza ajali za
vyombo hivyo ambazo zimekuwa zikigharimu maisha ya wanawake, watoto
pamoja na jamii nzima. Akizindua mradi huo Makao Makuu ya Ofisi za
TAMWA, Sinza jijini Dar es Salaam Kamanda wa Polisi wa Kikosi cha
Usalama Barabarani, Mohammed Mpinga amepongeza jitihada hizo kwani
zitasaidia kuongeza elimu juu ya masuala ya usalama barabarani na namna
ya kukabiliana na ajali.
Akizungumza awali Mkurugenzi
Mtendaji wa TAMWA, Bi. Edda Sanga alisema chama hicho kimeguswa
kushiriki katika mapambano ya ajali za barabarani kutokana na kuona ipo
idadi ya wanawake wengi na watoto wamekuwa wakiathiriwa na ajali hizo
kila uchao. Alisema ujio wa usafiri wa pikipiki maarufu kama bodaboda
watumiaji wengi wa usafiri huo ni wanawake wanapokuwa katika shughuli
zao za kila siku na ndio wanaoguswa na ajali hizo.
Alisema wapo wakina mama ambao
wamekuwa wakifanya biashara zao pembezoni wa barabara kundi ambalo nalo
limekuwa likiathiriwa kwa kiasi kikubwa na ajali za barabarani
zinapotokea. Akifafanua zaidi alisema chama hicho kitajikita katika
kutoa elimu ya usalama barabarani; ikiwa ni pamoja kupinga ulevi wakati
wa uendeshaji vyombo vya moto, kuhamasisha uvaaji wa kofia ngumu
(helment) kwa waendesha pikipiki pamoja na abiria wao, kuhamasisha
ufungaji mikanda kwenye magari pamoja na kuelimisha jamii kuwa mwendo wa
kasi barabarani ni hatari.
Kwa upande wake mgeni rasmi
katika tukio hilo, Kamanda Mohammed Mpinga alisema kuna kila sababu ya
wadau kama TAMWA kujitokeza kupambana na ajali za barabarani kwani
zinamguza kila mmoja. Alisema licha ya idadi ya ajali kuendelea kupungua
mwaka hadi mwaka ukilinganisha, lakini bado kuna roho na mali za raia
zinapotea kila wakati hivyo kuna kila sababu ya elimu ya usalama
barabarani na mapambano yakafanywa kwa ushirikiano wa wadau wote.
Alitolea mfano kwa kipindi cha
miezi sita kuanzia Januari 2016, jumla ya ajali za barabarani
zilizotokea ni 5,152, ambapo vifo vilikuwa 1,580 na majeruhi ni 4,659
huku vifo hivyo vikigharimu maisha ya wanawake 301. Uzinduzi huo ambao
uliambatana na kutoa mada mbalimbali juu ya mikakati na mapambani katika
mradi huo, wakiwemo viongozi wa Serikali, madereva na mashirika anuai
yasiyo ya kiserikali pamoja na waandishi wa habari.
0 comments:
Post a Comment