Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia,
Wazee na Watoto, Mh. Dk. Hamisi Kigwangalla amefanya ziara ya kikazi
katika Wilaya ya Mlele na kutembelea Hospitali ya Mlele ya Wilaya hiyo
pamoja na Hospitali ya Mpanda iliyopo Wilaya ya Mpanda Mkoani Katavi
huku akitoa maagizo mbalimbali ya kiutendaji.
Katika ziara yake katika Hospitali ya Mlele,
Dk.Kigwangalla amewaagiza viongozi wa Serikali wa Wilaya na ule wa
Hospitali hiyo kuhakikisha wanakamilisha mambo muhimu ikiwemo ujenzi wa
chumba cha upasuaji, jengo la kuhifadhia mahiti na vitu vingine huku
akitaka ndani ya miezi mitatu view vimekamilika.
Akiwa katika Hospitali hiyo ya Mlele,
Dk.Kigwangalla ameweza kutembelea sehemu mbalimbali za hospitali pamoja
na kukagua ujenzi wa majengo ya Chumba cha upasuaji, chumba cha
kuhifadhia maiti na majengo mengine ambapo amemtaka Mkuu wa Wilaya
kuhakikisha wanafanya juhudi wanakamilisha kwa wakati majengo hayo ili
wananchi wapate huduma bora.
Kwa upande wa ziara yake hiyo katika Wilaya ya
Tanganyika yaliyopo makao makuu ya Mkoa wa Katavi, Dk. Kigwangalla
ameweza kutembelea Hospitali ya Mpanda ambayo kwa sasa inahudumia kama
Hospitali ya Mkoa ambapo napo ameagiza kufanyiwa marekebisho mbalimbali
ikiwemo kuzingatia masuala usafi.
Aidha, ametoa maagizo kuhakikisha wanafunga mfumo
wa malipo wa kisasa katika vyanzo vyote vya mapato ili kukusanya pesa
nyingi zaidi zitakazoweza kuendesha huduma za Afya ndani ya Hospitali
hiyo.
0 comments:
Post a Comment