Watu tatu wamefariki Dunia
huku wengine 28 wakijeruhiwa, baada ya daladala waliyokuwa wakisafiria
kugonga Treni ya abiria katika eneo la Tanesco Manispaa ya Morogoro,
huku idadi hiyo ya Majeruhi wengi wao wakiwa ni wanafunzi wa Shule za
Sekondari Tushikamane, na Mji Mpya.
Ajali hiyo imetokea majira ya
saa moja na nusu asubuhi ikihusisha Daladala lenye namba za usajili T
438 ABR na ilikuwa imebeba Abiria 31, huku wakiwamo wananfunzi hao ambao
walikuwa wakielekea shuleni.
Kwa mujibu wa kamanda wa
polisi Mkoa wa Morogoro Ulrich Matei, amesema chanzo cha ajali hiyo ni
uzembe wa Dereva wa daladala hiyo, ambaye alijaribu kulazimisha kuvuka
kwenye kivuko cha Treni kilichopo katika eneo hilo, licha ya kupewa
ishara ya ujio wa Treni hiyo ya Abiria iliyokuwa ikitokea Kigoma, na
ilipofika katikati, daladala hiyo ilizima na kugonga upande wa ubavu na
kupelekea vifo hivyo.
Kwa upande wake Mganga Mkuu
wa Mkoa wa Morogor Dr Jacob Frank, amekiri kutokea kwa vifo hivyo na
kupokea majeruhi 28, ambao wanaendelea kupatiwa Matibabu katika Hospital
ya Rufaa ya mkoa wa Morogoro.
Baada ya kutokea kwa ajali
hiyo Dereva wa Daladala hiyo alijaribu kutoroka, hata hivyo wananchi
walifanikiwa kumkata na kumshushia kipigo, kilichompatia majeraha
kadhaa, ambapo alikimbizwa katika Hospital hiyo kwa matibabu zaidi.
0 comments:
Post a Comment