Chama cha
Demokrasia na maendeleo( Chadema ) kimeandaa semina ya siku mbili (2) kwa
viongozi ili kuwajengea uwezo na ufahamu
wa kutenda kazi zao ndani ya chama, viongozi hao ni wa chama na madiwani wake.
Akiongea na
MALAFYALELEO mwenye kiti wa chama hicho mkoa wa Mbeya PETER K MWAMBONEKE
amesema wameamua kufanya semina hiyo kwa viongozi na madiwani wa chama hicho wa
mikoa mitatu ikiwemo RUKWA, RUVUMA na MBEYA ili kuwapa uwezo na ufahamu
viongozi wake wa kujua wajibu wao katika kufanya kazi za chama.
Na kwa
upande wa madiwani kujua majukumu yao kwa Halmashauri na wananchi walio
wachagua ili wawatumikie
Semina hiyo
imeanza tarehe 12-13/06/2012 maeneo ya sokomatola katika ukumbi wa MKAPA jijini
MBEYA.
Wakufunzi wa
semina hiyo ni;
1.
BENSON
S. KIGAILA (Mkurungenzi wa mafunzo)
2.
LAZARO
T. MAASAY (Mwenyekiti wa Halmashauri Karatu) Pia mjumbe kamati kuu.
3.
SHABANI MBAMBO (Meya Kigoma)
4.
ERASTO
NDENKA (Program officer wa KONRAD ADONAYER STIFTUNG(KAS)
Mafunzo hayo yamedhaminiwa na chama cha demokrasia na maendeleo (Chadema) Taifa kwa
kufadhiliwa na shirika la KONRAD ADONAYER STIFTUNG (KAS) la jijini
Dar-es-salaam.
Program officer wa KONRAD ADONAYER STIFTUNG (KAS) ERASTO NDENKA akitoa mafunzo kwa washiliki wa semina na viongozi wa (chadema) Picha na charles mwaipopo.
Mwenyekiti wa chadema mkoa wa MBEYA PETER K. MWAMBONEKE akiuliza swali kwa mwezeshaji wa semina.(Picha na charles mwaipopo)
Baadhi ya viongozi na madiwani walioshiriki semina hiyo (Picha na charles mwaipopo)
Huu ndo ukumbi mdogo wa kumbukumbu ya Rais Benjamin Mkapa Wanako fanyia semina hiyo (Picha na charles mwaipopo)
0 comments:
Post a Comment