Jinamizi la
ajari lazidi kulikumba Jiji la Mbeya ni mara baada ya basi doga aina ya Hiace yenye namba za usajili T247 BUF Linalo milikiwa na Huruma mwakasa maarufu( Daladala) lililokuwa likifanya safari
zake kati ya mwanjelwa na mbalizi kuligonga
Lori kwa nyuma lenye namba za usaji T 786 BBH Linalomilikiwa na kampuni ya
malumalu jijini hapa, Na kusababisha watu zaidi ya (20) kujeruhiwa vibaya
Ajali hiyo
imetokea alfajiri ya leo jun 14/2012 maeneo ya Ituta Iyunga barabara ya Mbeya
na Tunduma.
Chanzo cha
ajari hiya kwa mujibu wa abiria ni mwendo kasi wa Dereva ambeye hatukupata majina yake kushindwa kulimudu gari
hilo na kuligonga lori hilo lilikuwa limeegeswa pembeni mwa barabara.
Ajali hii
imekuja mara tu wananchi na wakazi wa Jiji la Mbeya bado hawajasahau machungu ya
Ajali mbaya ya coster iliyokuwa ikitoka Mbeya kwenda Kyela kugongwa na lori la
mizigo, iliyopoteza maisha ya ndugu jamaa na marafiki na wengine kupata kilema
cha maisha iliyotokea hivi karibuni maeneo ya uyole Mbeya vijijini.
0 comments:
Post a Comment