Mwananchuo wa chuo
cha ualimu cha ST Aggrey kilichopo uyole
jijini mbeya anasadikiwa kufariki
dunia baada ya kupigwa na
wananchi wenye hasira kali katika maeneo
ya Isanga kwa tuhuma zakuiba pikipiki
zakusafirishia abiria maarufu kama
bodaboda.
Mmoja wa mashuhuda wa tukio hilo PRAY GOD MGONJA
amemtaja mtuhumiwa huyo kuwa ni VEDASTO PIUS anayekadiriwa kuwa na umri
kati 25 mpaka 30 .
Mgonja amesema tukio hilo limetokea mnamo july 2 mwaka huu majira ya saa 8 za mchana katika daraja lilopo karibu na hotel ya Rift Valley barabara
yakuelekea isanga jijini mbeya.
Amesema mtuhumiwa
amekumbwa na mkasa huo baada yakupewa
taarifa za kuibiwa kwa pikipiki yenye No T 438BZU aina T-BETTER yenye alama ya
chama cha Demokrasia na maendeleo mali
ya JOSEPH KAPASI(23)mkazi wa Ilomba
jijini hapa.
Kwaupande wake
mmiliki wa pikipiki hiyo JOSEPH KAPASI amesema aliombwa kumfundisha mtuhumiwa
huyo na baadae alipoanza kuendesha vizuri alitokomea nayo na marabaada
ya hapo alipatikana eneo la isanga akielekea barabara ya chunya ili aibe
na ndipo akakamatwa na wanainchi wenye hasira kali nakuanza kumpa kichapo
ambacho kimemfanya azirai.
TUNAOMBA LADHI KWA PICHA UTAKAZOZIONA KATIKA HABARI HII
Vedastos Pius akiwa amelala chini baada kupata kichapo kwa tuhuma za wizi wa pikipiki
Kitambulisho chake cha Aggrey Teachers College
Picha yake kabla ya kupata kichapoMwandishi wa Blogg hii Charles Mwaipopo Akimhoji Praygod aliyefanikisha kumkamata anayetuhumiwa kwa wizi wa pikipiki





0 comments:
Post a Comment