Naibu waziri
wa elimu na mafunzo ya ufundi Mh.
PHILLIP MULUGO amewataka walimu kubadilika katika utendaji wao wakazi katika
mwaka wa fedha wa 2012 ili kuendeleza elimu nchini.
Mulugo
amesema hayo wakati wamkutano na wadau
wa elimu kutoka maeneo mbalimbali mkoani
mbeya wakiwemo maafisa elimu
,waku shuele za sekondari na maafisa taaluma.
Amesema mtu
yeyote atakayezembea kufanya kazi katika wizara yake atafukuzwa kazi kwani kuwakumbatia wafanyakazi wazembe ni kuzorotesha maendeleo nchini nakuwataka walimu na viongozi wao kufanya
kazi kwa bidii ili kupunguza kero ambazo wizara ya elimu inazokumbana nazo.
Hata hivyo
ametangaza kiama kwa wafanyakazi ambao wanaiba vitendea kazi vya shule nakuiba
mitihani ili wanafunzi wafaulu
atawajibisha kwakuwakamata kuwapeleka mahakamani ili sheria ichukue
mkondo wake nakufunga shule ili
kukomesha vitendo hivyo Pia amewataka walimu kuacha maramoja vitendo vya
kuwatuma wanafunzi kuwaandikia wenzao nots ubaoni sana katika shule za
sekondari atakaye kamatwa akifanya hivyo
atawajibishwa.
Katika hatua
nyingine amewatoa hofu walimu kuhusu suala la uhamisho kwamba kuanzia mwaka huu
wa fedha litashughulikiwa na mkurugenzi wajiji
kwani wao ndio wanaofahamu walimu
kuliko wizarani nakuongeza kuwa mtindo
huo utasaidia kuepukana na malalamiko
ambayo walimu wanakumbana nayo katika
uhamisho.
Aidha
ameaasa viongozi mbalimbali ambao wanawajibu wakuwateuwa nakuwapandisha vyeo walimu kuacha kutumia
mwanya waukabila kwani wakigundulika wizarani watapangua uteuzi huo na kuteua
upya ili kukomesha ukabila katika kazi
ambao unaharibu maendeleo ya taifa.
0 comments:
Post a Comment