Pages

Ads 468x60px

Thursday, July 5, 2012


MAUAJI  MBOZI
3/7/2012
Mganga mmoja wa tiba ya asilia  aliyefahamika kwa jina la Mwendapandi Mwafogo(78) ameuawa na watu wasiofahamika katika kijiji cha Sesanga Wilayani Mbozi  Mkoani Mbeya kwa tuhuma za kishirikina.

Kamanda wa polisi mkoani mbeya Diwani Athumani amesema tukio hilo limetokea  mnamo july 3 mwaka huu majira ya saa nne za asubuhi katika kijiji cha Sesanga wilayani humo.

Athumani amesema kuwa mwili  wa marehemu ulikutwa umetupwa katika mto Harungu  ukiwa umenyogwa  na jeraha kubwa usoni, huku  mikono na miguu ikiwa imefungwa kwenye baiskeli yake.                                           

Hata hivyo Bw.Diwani amedai kuwa  marehemu anatuhumiwa kuwa  mchawi kwani alikuwa  anawasaidia wachawi kuloga watu kijijini hapo.

 Aidha Bw.Diwani ameitaka jamii kuondokana na imani potofu za kishirikina  ikiwa ni pamoja  na kutojichukulia sheria mkononi.      

ILOLO  JIJINI MBEYA
3/7/2012
Mtoto mmoja aitwaye Bonifance  Edward mkazi wa kijiji cha Ilolo  jijinj Mbeya amefariki dunia baada ya kutumbukia kwenye shimo la maji machafu wakati akicheza na watoto wenzake.

Kamanda wa polisi mkoani Mbeya Bw.Diwani  amesema tukio hilo limetokea julai 3 mwaka huu majira ya saa nane mchana katika eneo la Ilolo jijini hapa.

Diwani amesema kuwa mwili wa marehemu umehifadhiwa katika hospitali ya Rufaa mkoani Mbeya.


Katika hatua nyingine  Bw Athumani amewataka wazazi na walezi kuhakikisha mazingira yanayo wazunguka watoto na jamii kwa ujumla kuwa salama ili kuepukana na matatizo kama hayo.
xxxxxxxxxxxxx  JULIANA   na RESTITUTA. xxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxx


xxxxxxxxxxxxxxxJULIANA na RESTITUTAxxxxxx

0 comments:

Post a Comment