UMOJA WA MAAFISA ELIMU TANZANI (UMET)
WAKAZA BUTI KUPAMBANA NA CHAMA CHA WALIMU TANZANIA (CWT)
Wasema hawako tayari kuunga mkono
maandamano yanayopagwa na chama hicho kwani CWT na Serikali wote ni waporaji wa
haki za waalimu.
Akiongea
Katibu wa umoja huo Meshaki Kapange katika mkutano wao uliofanyika katika
ukumbi wa kiwira hotel Soweto iliyopo jijini Mbeya Amesema kuwa lengo la mkutano
huo ni kuwajuilsha walimu juu ya hoja zao 19 walizopeleka Bungeni, kupitia Kikao
kati ya UMET na Kamati ya Bunge ya kudumu ya huduma ya jamii kilicho fanyika may
28 mwaka huu katika ukumbi wa Wizara ya maendeleo ya jamii na watoto.
Akizungumzia
kuhusu kupinga mgomo unaotangazwa na kuandaliwa na chama cha waalimu Tanzania
CWT na kutoa tamko na msimamo wa UMET amesema
kuwa CWT na Serikali wote kwa pamoja wanatakiwa kugomewa kwakuwa ni waporaji wa
haki za waalimu kwani Wenye haki ya kugoma ama kutogama ni waalimu wenyewe, hivyo
UMET utaendelea kutoa Elimu kwa waalimu kujua haki zao zinazoporwa.
Mwisho wa
kikao hicho ilikuwa ni kuchagua viongozi wa Wilaya ya Mbeya jiji, na Mbeya
vijijini.
0 comments:
Post a Comment