KAMANDA WA
POLISI MKAONI MBEYA DIWANI ATHUMANI AMEKIRI KUWEPO KWA UVUNJAJI WA SHERIA ZA
USALAMA BARABARANI KWA MADEREVA WA DALADALA MKOANI HAPA.
Akiongea na
mwaandishi wa blog ya Malafyaleleo kwa
njia ya simu, Kamanda amesema wamejipanga vilivyo kukomesha madereva wote
watakao endelea kuvunja sheria za barabarani kama ilivyo sasa.
Amesema ameanza kuwaondoa wapigadebe wanaowasumbua
Abiria wanaotumia usafili huo, na kisha rungu litaelekea kwa madereva wazembe.
Kwa upande wao madereva ambao hawakutaka kutajwa majina yao
wamekili kuwepo kwa vitendo hivyo na kuongeza kuwa wanafanya hivyo ili kupata
abiria nakutimiza malengo tajiri.
“Big usopochukua
mtu wrongparking huwezi kupata malengo ya tajiri na wewe kupata posho ya
kijikimu na familia yako, ukiaacha kuchuku anayekuja nyuma anachukua kwa hiyo
inakulazimu uchukue tu” alisema mmoja wa madereva hao
Hata hivyo
wamesema mkuu wa polisi usalama barabarani mkoani mbeya aliyepita maarufu kwa
jina la OBAMA aliweza kudhibiti vitendo hiyvyo kwasababu alikuwa anashinda
barabarani.
“Unajua
Obama saa kumi na mbili alikuwa barabarani kwa hiyo kuvunja sheria huwezi kwani
ukifanya hivyo unakuta ametokea, Yule
bwana utafikilia alikuwa mchawi, Huyu mama yeye anashinda ofisini tu ni
malachache sana hutokea barabarani na akikukamata anakuonya na kukuruhusu
uondoke ndiyo maana watu wanavunja sheria”alisema mmoja wa madereza hao.
Kumekuwa na kasumba kwa madereva wa mabasi
madogo maarufu kama daladala mkoani hapa kutofuata sheria za usalama barabarani
ikiwemo kuchukua abiria sehemu isiyokuwa na kituo maalumu maarufu kama wrongparking,
kuegesha magari yao katika stendi bila kuacha nafasi ya kupita mtumiaji
mwingine wa barabara marufu kama double paking na hivyo kusababisha usumbufu
kwa watumiaji wa barabara wengine.
0 comments:
Post a Comment