Muungano
wa jamii Tanzania (MUJATA) umemuomba
radhi mkuu wa mkoa wa mbeya Mh.ABBAS KANDOLO kuwa hakupaswa
kushutumiwa na wananchi mkoani hapa kuwa alihusika na vurugu za machinga zilizotokea mwaka jana.
Hayo yamesemwa katika mkutanao uliofanyika Inyala wilaya ya mbeya vijijini uliowakutanisha machifu wote wa mkoa wa mbeya,
mwanza,shinyanga,Luvuma na Rukwa wenye lengo lakupinga vikali vitendo viovu vinavyotendwa na watu wasioutakia mema
mkoa wa mbeya.
Wamesema mkuu wa mkoa wa mbeya ABBAS KANDOLO anastahili kuombwa radhi kwani wakati wa vurugu za mwanjelwa alikuwa mgeni katika mkoani hapa hivyo kumuhusisha na na vurugu ni kumuonea.
Hata hivyo wametaja baadhi ya vitendo vingi vya uvunjifu wa amani mkoani
hapa kuwa ni pamoja na upigaji nondo,kuzika
watu wakiwa hai ,siasa za uchochezi
hali inayosababisha maandamano na
uharibifu wa rasrimali ukiwemo uchomaji
wa barabara.
Mwenyekiti wa machifu mkoa wa mbeya SHAYO SOJA MASOKO
amewaomba wananchi mkoani hapa kushiriki
katika ulinzi shirikishi ili kuondokana na vitendo hivyo nakuongeza kuwa
vitendo hivyo vinauletea sifa mbaya mkoa huu.
Pia amesema kitendo chakufanya jaribio lakumzika chifu
melele ambayo aliokolewa na jeshi la polisi na watu wengine wa wa wili ambao
wamezikwa eneo la itezi uyole na malamba
wilayani mbarali kwa tuhuma
zakishirikina.
Amesema matukio hayo yanaendelea kushamili kutokana na baadhi ya watu baada yakufiwa na
ndugu zao wanaenda kwa waganga wa kinyeji
kupiga lamuli ili kujua aliehusika na kifo cha marehemu na hatimaye huambiwa
kuwa mtu Fulani hivyo kusababisha matendo hayo kuibuka siku hadi siku.
Kwaupande wake
mkuu wa wilaya ya mbeya NOMANY SIGARRA AMBAYE alikuwa mgeni rasmi katika
mkutano huo kwa niaba ya mkuu wa mkoa wa mbeya
amewapongeza viongozi wa ulinzi shirikishi na muungano wa jamii (MUJATA)
kwa kuwa mustali wa mbele kulinda na
kupigania haki mkoani hapa.
Amesema serikali
iko tayali kuunga mkono chama
chochote , taasisi ya dini ama kikindi
chochote kinachopigania amani kwani ni
wajibu wa serikali kutetea wananchi wake.
Akizungumzia kuhusu msamaha wa mkuu wa mkoa wa mbeya
Mh. ABBAS KANDOLO amesema mkuu
huyo ameshasamehe mda mrefu na hana
kinyongo na mtu yeyote Yule kuhusu suala hilo.
Aidha amesema chama chochote ambacho kinapanda jukwaani
kutukana matusi kitachukuliwa hatua kali za kisheria kwani kufanya hivyo ni
kesi ya jinai nakuongeza kuwa polisi itamushughulikia mwanachama yeyote atakaye
jaribu kufanya hivyo.
Mkuu wa Wilaya ya Mbeya Nomany Sigarra akisisitiza jambo katika mkutano huo
Mwenyekiti wa machifu Mkoa wa Mbeya Shayo masoko akielezea kitu wakati wa mkutano.
Mwenyekiti wa ulinzi shilikishi Kaijage akikemea vitendo vya uzikzji watu wakiwa hai
Chifu Matuge akiwa katika pozi la utulivu akiendelea kusikiliza mkutano
Mkuu wa wilaya ya Mbeya Nomany Sigarra akicheza ngoma za kienyeji zilizokuwa zikitumbuiza katika mkutano.
0 comments:
Post a Comment