Chama
cha demokrasia na maendeleo CHADEMA kimeendelea kuinyama raha CCM baada ya kunyakua
viti sita kati ya saba vya uenyekiti wa serikali za mtaa na viti nane kati ya
14 vya wajumbe katika kata mbalimbali zilizoachwa wazi jijini mbeya.
Hayo yamesemwa na mwenyekiti wa chama hicho wilaya ya
mbeya mjini JOHN MWAMBIGIJA wakati akizungumza na waandishi wa habari katika
ofisini za chadema zilizopo manga jijini hapa.
MWAMBIGIJA amesema hii ni ishara tosha ya kukiondoa
chama cha mapinduzi madarakani kwani
wao ni waasisi wakukiondoa chama hicho
kikifuatia na vyama vingine ambavyo vipo nchini.
Katika majigambo yake amesema CHADEMA ni Barcelona na
CCM ni mtibwa hivyo wataendelea kuangusha kichapo dhidi yao katika kampeni yao ya twanga kotekote akiliita ni
jeshi la NATO hivyo CCM haina pakuchomokea.
Katika uchaguzi huo ambapo wenyeviti ni Richard A
mwakalinga mtaa wa benki kata ya Rwanda Willy Chaula mtaa wa karobe kata ya
karobe, Ngambi kulagha mtaa wa ilolo
kata ya manga,James mwakalobo mtaa ilemi kata ya ilemi,phillipo mwalukisi mtaa
wa tembela Josephat hasara Gunga wa mwanseko.
Na kwaupande wa wajumbe ni Eneya mwansojo mtaa wa ilolo
kati ,mtaa wa ilemi Benjamini mbwilo ,Erick Legembo wa mtaa wa mwanseko na
wengineo wengi.
Pia amesema
viongozi hao wamechaguliwa ili kuziba nafasi ambazo ziliachwa na watu ikiwemo
kuhama vyama na wengine kupoteza maisha kutoka
vyama mbalimbali jijini hapa.
Mwenyekiti wa Chadema Wilaya ya mbeya mjini John Mwambigija akizungumza na waandishi wa habari katika ofisi za chadema.
0 comments:
Post a Comment