KANISA
LA KIINJILI LA KILUTHERI TANZANIA
|
TAMKO LA DODOMA
MSIMAMO
WA KANISA LA KIINJILI LA KILUTHERI TANZANIA KUHUSU NDOA ZA JINSIA MOJA.
1. Utangulizi
1.1 Kanisa la kiinjili la kilutheri Tanzania
(KKKT), Linamshukuru mungu kwamba katika hekima yake isiyopimika, na kwa njia
ya mwana wake Yesu Kristo ametuunganisha waumini wake wote ulimwenguni kuwa
mwili mmoja na hivyo kutufanya tuhusiane. Kwa kwa njia hiyo tunaweza kutembea
pamoja na kufanikishwa katika mambo mengi.
1.2 katiak
uhusiano wetu kama mwili mmoja tumeshilikiana katika mambo magumu na mepesi
kilichotuwezesha kudumu pamoja hadi sasa, kwa msaada wa mungu, ni kutambua na
kukumbuka kwamba kila siku ya ibaada, tunakili kuwa kanisa la mungu ni moja,
takatifu ulimwengu pote na la kimitume.
Hivyo, tukio lolote katika kanisa mojawapo, lisilo la kawaida katika misimamo
na mafundisho yaliyozoeleka kwa karne nyingi katika kanisa la mungu,ni lazima
litaamsha mshtuko na itikio la aina moja au nyingine kutoka makanisa mengine
duniani pote.
1.3 Kwa
wakati uliopo. Mojawapo ya matukio yasiyo ya kawaida, kwa mtazamo na
uelewa wa KKKT, ni hilo la baadhi ya
makanisa - hasa kule ulaya na Marekani – kuamua kuhalalisha ndo za watu
wa jinsia moja katika kufanya hivyo,sababu mbalimbali zinatolewa na makanisa
husika uwamuzi wao huo. Hapa tutaje tu, kwa muhtasari baadhi ya sababu zinazo
tolewa na makanisa hayo.
1.3.1 Kwamba
eti mafundisho ya kanisa kwa ndoa, kulingana na maandiko matakatifu, ni kati ya mwanaume na mwanamke si kama
inavyo fafanuliwa. kwa msingi wa hoja kama hii, hao wanao tetea ndoa za watu wa
jinsia moja wameanza kusama kila linalo wezekana kubomoa kifungu kimoja baada ya kingine kinachoonyesha kwamba ndoa halali, kibablia,
ni kati ya mwanaume na mwanamke. Wanafanya hivyo kwa kuleta tafsiri zao “ mpya
na yamkini potofu” – tofauti na msimamo wa kanisa uliodumu kwa
miaka mingi kuhusu maana ya ndoa
kulingana na mafundisho ya neno la mungu. Baadhi ya vifungu vya Biblia vinavyo
pigwa vita na kupewa tafsili
nyingine na wapenda ndoa za watu wa
jinsia moja ni hivi vifuatavyo: Mwanzo 1:26-28; 2: 24;
Mt. 19:
5-6a; Rum. 1:26-27a na Gal. 3:28
1.3.2 Kwamba
eti kilicho muhimu, kwa habari za mahusiano kati ya wawili wahusika katika
mahusiano ya kindoa au namna nyingine za mahusiano ni upendo. Mradi watu wanapendana, mahusiano
kamahayo ni sahihi na halali ndivyo wanavyodai watetezi wa ndoa kati ya watu wa
jinsia moja.
1.3.3 Kwamba
eti mazingira na tamaduni zao za wakati huu ni tofauti na zawakati uliopita
kuhusu maana na mtazamo juu ya nini halali na nini si halali kwa mahusiano ya kindoa na kimapenzi.
Wanaongeza kudai kuwa swala la maadili kuhusu nini ni dhambi na nini si dhambi,
hubadilika kulingana na wakati na mazingila ya mahali mtu alipo. Kwa macho yao,
mtazamo wa jamii juu ya maadili, hasa kuusiana na swala la mahusiano ya kindoa
au kimapenzi kati ya watu wa jinsia moja au jinsia tofauti umebadilika, na
wanalitaka kanisa nalo liende na wakati katika mtazamo ama msimamo wake kuhusu
mambo haya . kadhalika wateteaji wa mambo wanadai kwamba, “tabia za kukemea na kukunjia uso mambo
ya ndoa za watu wa jinsia moja zimepitwa na wakati,” Hivyo , wanatutaka
sisi wengine wote katika kanisa la mungu na jamii ya
ulimwengu kwa ujumla tukubali kubadilika na kwenda na wakati, kama wao, katika
mazingila haya mapya!
1.3.4 Kwamba
eti kwa kuwa sheria za nchi hizo yaliko makanisa yanayo tetea na kuhalalisha
ndoa za watu wa jinsia moja zimebadilika na kuwa upande wa ndoa za aina hiyo,
makanisa katika nchi hizo yangejikuta pagumu sana katika kazi na maisha yao
kama yangeng’ang’nia msimamo wao wa miaka yote iliyopita kuhusu ndoa kati ya
watu wa jinsia moja, na maswala mengine ya mahusiano kati ya watu wa jinsia
hiyo moja. Maana yake, kwa tafsiri yetu, makanisa hayo yameamua kukabiliana na
hatua zilizochukuliwa na mamlaka ya nchi zao kama njia ya majadiliano ili hayo
makanisa yasije yaka poteza maslahi yao fulan katika swala zima la ndoa endapo
yangeendelea kushikilia msimamo wao wa miaka yote iliyopita – yaan, kupinga na
kukataa uhalali wa ndoa za watu wa jinsia moja.
1.3.5 Kwamba
eti suala la mahusiano – kindoa au kujamiiana ki-namna nyingine – kati ya watu
wa jinsia moja, ni uamuzi wa kati ya watu wawili wanaohusika; wana uhuru kuamua
kufanya wapendavyo katika hili. Kwahiyo dai la msingi ni kwamba siyo sawa kwa
yoyote kuwaingilia katika mambo yao hayo, bali kuwaacha huru wafanye
wapendavyo. Na makanisa yaliyo halalisha ndoa za watu wa jinsia moja.
2. HOJA MBADALA
2.1kuhusu
hoja zitolewazo na watetezi wa ndoa za watu wa jinsia moja, Kanisa la kiinjili
la kilutheri Tanzania lina mtazamo na msimamo tofauti. Halikubaliani na sababu
zozote zinazotolewa watetezi wa ndoa za aina hiyo na uhalalishwaji wake.
2.2 Kanisa
hili, (KKKT), Linasimama juu ya msingi wa neno la mungu kwamba maana ya ndoa ni
kama inavyo fundishwa katika vifungu vya Biblia vilivyo tajwa sehemu ya 1.3.1
hapo juu. Vifungu ambavyo vimeanza kupewa maana na tafsiri tusiyoweza kuikubali. Sisi na wengine wote duniani pote wlio na msimamo kama wetu katika
swala hili la kupinga ndoa za watu wa jinsia moja, tunaamini kuwa Biblia
haitafsiriwi ka wapendavyo watu Fulani au mamlaka Fulani ama utamaduni Fulani
bali hujitafsiri yenyewe kwa rugha
mbalimbali kwa usahihi wake usio badilika
2.3 Kanisa
hili linaamini kwamba upendo ni kiini cha mapenzi na uhusiano wa kweli Kati ya watu
wawili wanaoishi, au wanotaka kuishi pamoja, katika ndoa. Lakini, kwa habari ya
kuolewa na kuoa, upendo huu ni kati ya watu wawili wa jinsia tofauti. Aidha
KKKT inaelewa somo juu ya upendo ni pana sana, na kwamba kuna maadili maalumu
kuhusu matumizi sahihi ya karama hii ya upendo
ua kupendana.
Kanuni maadili kuhusu maana sahihi ya upendo na matumizi yake zinapokiukwa ua
kuanza kupindishwapindishwa kwa sababu yoyote ile, basi upo uwezekano mkubwa wa
binadam kujikuta katika hali ambayo neno upendo upo kati ya watu wawili wahusika,
basi ndoa ya aina yoyote inakubalika . Hoja hii ikikubalika kanisa na jamii kwa
ujumla tunaweza kujikuta mahali ambapo tunaanza kurudia na kutetea ndoa hata
kati ya wana na ndugu, wazazi na watoto napengine hata kati ya binadam na
wanyama – si mladi kinachowaunganisha hao viumbe wawili kinaitwa upendo!
Haidhuru ni tafsiri gani imetolewa? Tunacho taka kusisitiza hapa ni kwamba,
tuwe waangalifu sana tunapo zungumzia neno upendo ha kudiliki kufanya kuwa kigezo
muhimu na pekee kuliko vyote katika swala la ndoa.
2.4 Jibu
liliotangulia, hapo juu, linahusu pia uhalalishwaji na ushabikiaji wa ndoa za
watu wa jinsia moja kwa hoja kwamba katika tamaduni na jamii za watu wa nchi zile
ambako ndoa za jinsia moja zimehalalishwa, pamekuwepo na mabadiliko makubwa
katika fikra za watu. Watu hawaonitena kwamba ni vibaya wala kutokuwa halali
kwa watu wa jinsia moja kuoana. Utamaduni wao wa sasa una mwelekeo unaoungua
mkono ndoa za jinsia hiyo. Mtazamo wa kimaadili wa sasa ni tofauti na wakati
uliopita. KKKT inakubali kuwa nikweli misimamo Fulani ya kimaadili inaweza
kubadilika kulingana na watu wako wapi na niwakati gani. Lakini waumini wa KKKT
wanajua na kuamini kuwa kuna mambo yasiyo badilika kama pua kutobadilika kuwa
mdomo au masikio kuwa macho.
2.5 Ni kweli
kuwa maadili yaliyo angaliwa na jamii kwa mwelekeo hasi miaka iliyo, sasa
yaangaliwa kwa mwelekeo wa chanya au kulidhia. Ni dhahili kuwa wakani wa sasa
na tofauti, na jamiiimebadilika katika mwelekeo na mtazamo wake katika mambo
mengi. Lakini ni kweli, vilevile, kwamba maadili na msimamo wa kanisa na wa
jamii kwa ujumla, haviwezi kuwa na misingi ya kimaadili inayo yumbayumba wakati
wote. Ni lazaima na jamii viwe na kanuni za kimaadali zinazoweza kihimili
mabadiliko ya kijamii, kisayansi, kisiasa, kiuchumi, nk.kanisa hili linaamini
kuwa, kwa msingi wa mafundisho ua neno la Mungu, yako maadili yasiyopaswa
kubadilishwa na kupindishwa pindishwa na misukumo ya mabadiliko ya wakati, hali
na mali.Mojawapo katika hayo, yahusu suala la ndoa na maana yake.Aidha kukubali
ndoa za watu wa jinsia moja ni kuhujumu msingi wa agizo la Mungu kuhusu uumbaji
unaoendelea.
2.6 Aidha,
mabadiliko ya kimaadili katika jamii moja, mahali Fulani, tuseme Ulaya na
Marekani, yasichukuliwe kama ndio mwongozo kwa mabadiliko mahali pengine pote
ulimwenguni. Wala mabadiliko yao ya kitamaduni, kijamii, nk, katika nchi za
Ulaya na Marekani yasilazimishwe juu ya watu wa nchi nyingine au makanisa
katika nchi hizo. Kwa sababu hao watu wa sehemu nyingine, nje ya Ulaya na
Marekani, pia wanamisingi yao kijamii inayolinda maadili yao. Sisi kama
watanzania/Waafrika, tuna maadili yetu yaliyojengwa juu ya misingi ya tamaduni
zetu bayana ambazo zinatambua mahusiano, ki – ndoa, kati ya watu wa jinsia
tofauti. Kwa hiyo, kama watu wengine watasema kwamba wanahalalisha ndoa za watu
wa jinsia moja kwa kuwa mazingira mapya ya mahali na wakati walipo yanaruhusu
hayo, basi ieleweke kuwa mazingira ya wakati na tamaduni zetu hayaruhusiwi
mambo hayo
2.7 Hoja ya
kwamba ndoa au mahusiano kati ya watu wa jinsia moja ni jambo la watu wawili ,
ni hoja ya upande mmoja. Kwetu sisi waumini wa KKKT kwa upande wa pili
tunabainisha kuwa hilo siyo tukio kati ya watu wawili tu bali inaeleweka daima
kuwa wao ni sehemu ya familia na jamii pana zaidi. Hao wawili hawawezi
kuruhusiwa kujifanya mambo hata yasiyokubalika na jamii, kwa kinga ya: “Tuache
peke yetu,msituingilie katika mambo yetu; haya ni mambo yetu wenyewe, na ni
uamuzi wetu wenyewe, kufanya tulivyoamua kufanya,” nk. Hapana! Katika Kanisa na
jamii kwa ujumla, kwa kadri tunavyohusika katika mazingira na utamaduni wetu,
kuna mambo ambayo binadamu yeyote, haidhuru yuko wapi, sharti atambue kuwa yeye
si peke yake na wala hapaswi kuishi kwa nafsi yake tu katika mambo yote na
wakati wote. Ndio ilivyo katika suala hili la ndoa za watu wa jinsia moja.
3. HITIMISHO
3.1 Kwa hiyo
basi, kwa msingi wa ufahamu wa kanisa moja, na kwa kuona ulazima wa kuongoza
kanisa Kichungaji, kwa kufuata ufahamu wa Neno la Mungu na maungamo yake.
Kanisa la kiinjili la Kilutheri Tanzania linapenda kuonyesha bayana msimamo wake wa sauti ya kinabii, kuhusiana
na suala la ndoa za watu wa jinsia moja,
kwamba ni msongo mwitu na mwiba mkali katika mwili wa Bwana Yesu Kristo (1 kor.
12: 12- 27) unaosababisha jeraha lenye maumivu makali kwa wana KKKT na wengina
wengi wa mahali pengine ulimwenguni pote wenye msimamo kama wetu katika suala
hili, katika ngazi mbalimbali za uhusiano na mfumo wa uongozi.
3.2 Kanisa la kiinjili la kilutheri Tanzania
linaona kuwa maamuzi yoyote ya upande mmoja yasiyoendana na uelewa na mtazamo
wa pamoja katika suala la ndoa kati ya
watu wa jinsia moja yanadhoofisha umoja wa kanisa lote kama mwili wa kristo.
3.3 Kanisa
la kiinjili la Kilutheri Tanzania bado linakataa utumiaji usio sahihi na
tafsiri potofu za maandiko Matakatifu ili kuhalalisha ndoa za watu wa jinsia
moja.
3.4
Tunaamini kwamba hakuna sehemu yoyote ya kanisa la Mungu inayoweza kufaulu kutatua
mambo yake yote peke yake, bila nguvu ya pamoja ya mwili mzima wa Kristo. Kama
isemwavyo: Umoja ni nguvu, utengano ni
udhaifu. Jambo hili la maamuzi kuhusu kuhalalishwa kwa ndoa za watu wa jinsia
moja, limeonyesha dhahiri kwamba nguvu ya umoja wetu imedhoofishwa.
3.5 Bila
shaka haitoshi wala haisaidii tukiishia katika kulaumiana na kuhukumiana
kutokana na tofauti zetu juu ya suala hili. Busara na hekima ya Roho Mtakatifu,
itusukume kuzama katika maombi, toba, kuendelea kushauriana, kuonyana na
kusaidiana katika roho ya upendo wenye misingi ya Neno la Mungu (Kol. 3:5 – 17)
3.6
Tunapenda kuwatia moyo na kuwaunga mkono kwa dhati wale wote, katika makanisa
yote ulimwenguni- wawe wengi au wachache wanaopinga, uamuzi wa kuhalalisha ndoa
za watu wa jinsia moja. Tunatoa wito kuwa, sisi sote kwa pamaja tuendelee kuwa
chumvi na nuru katika uhusiano wetu. Tukierekeza nguvu zetu katika kudumisha
umoja na ushilikiano kati yetu. Umoja utatuwezesha kutoruhusu tena hali
itayoleta majeraha zai kwenye mwili wa kristo, yaani kanisa.
3.7 Tunaona
kwamaba hizi ni nyakati za uovu unao tafuta kulididimiza kanisa la mungu. Kwa
hiyo tunatoa wito kwa waumini wote wa KKKT na makanisa mengine yenye msimamo
kama wetu kuomba kwa thati na kutunza ushuhuda wa mtu binafsi na wa kanisa la
mungu.
3.8 tunatoa
tahadhari kwa kila muumini wa KKKT kuwa makini sana katika kupambanua na
kuyakata mafundisho mageni ambayo yanaweza kupotosha kwa urahisi waumini katika
ulimwengu huu wa utandawazi.
3.9 Katika
hali halisi ya ushilikiano kati yetu na makanisa mengine ya Ulaya na Marekani,
Nahali pengine, msimamo wa kanisa hili umewekwa bayana katika majibu ya hojaji
iliyoandaliwa na fungamano la makanisa yo kilutheri duniani (FMKD)kuhusu
ubadilishanaji wa watumishi. Kwakuwa lengo la hojaji hiyo na maamuzi yatakayo
fanywa hatimaye na FMKD kutokana na majibu yaliyotolewa na makanisa mengine
wanachama yanayotuhusu sisi pia;
3.9.1 Sisi
KKKT kama wanachama tunasema kwamaba kanisa letu halitakuwa tayali kufanya
mabadilishano ya watu wanayojumuisha wale walio katika ndoa za jinsia moja au
wale wanao shabikia ndoa za jinsia hiyo na uhalalishwaji wake. kwa maneno ya
wazi zaidi, ni kwamba walio katika ndoa za jinsia moja, na wanaoshabikia ndoa
za jinsia hiyo na uhalalishwaji wake, hawakalibishwi katika kufanya kazi katika
KKKT. KKKT haitakuwa tayari kuhusu suala hili hata kwa ushawishi na ua
shinikizo la nguvu ya fedha.
3.9.2 Hata
katika ushilikiano wake na wengine kwa njia ya vyombo vya ushilikiano kama vile
LWF, WCC, LMC na/au mashirika mengine (ya kidini na yasiyo yakidini) n.k., KKKT
haitaunga mkono mbinu zozote za kujaribu kupiga debe na kuwapenyeza katika
mashirika hayo watu walio katika ndoa za jinsia moja au washabiki wa nda za
jinsia moja, na aina zote za vitendo vya ushoga.
3.10 KKKT
haiwezi kuwalazimisha watu wa Ulaya au Marekani, waone na kufanya kama sisi
katika swala hili la ndoa za jinsia moja, lakini inaweza kuwaeleza msimamo wake
kinaganaga kuhusu swala lenyewe. Inaamini kuwa upande mwingine pia utajali na
kuheshimu msimamo wake kama unavyo elezwa katika tamko hili. Aidha KKKT
inategemea kuwa marafiki zake, popote pale walipo, ambao, lakini, inatofautiana
nao sana sasa katika suala hili la ndoa za watu wa jinsia moja, hawajaribu- na
ingeomba wasijaribu- kwa namna yoyote ile, wakati wowote ule, mahali popote
pale, kuujaribu msimamo wake dhidi ya ndoa za watu wa jinsia moja,ikiwa ni
pamoja na vitendo vya namna zote za kishoga.
Maaskofu wa
KKKT
1.
Askofu
Dk. Alex malasusa Mkuu, KKKT
2.
Askofu
Michael Adam, KKKT Dayosisi Mkoani Mara
3.
Askofu
Paulo 1. Akyoo, KKKT Dayosisi ya Meru
4.
Askofu
Dk. Benson K. Bagonza KKKT Dayosisi ya Karagwe
5.
Askofu
Elisa Buberwa, KKKT Dayosisi ya kaskazini Magharibi
6.
Askofu
Zebedayo Daudi, KKKT Dayosisi ya Mbulu
7.
Asikofu
Andrew P. Gulle, KKKT Dayosisi Mashariki Ziwa Victoria
8.
Askofu
Thomas Laiser, KKKT Dayosisi ya kaskazini kati
9.
Askofu
Cleopa A. Lukilo, KKKT Dayosisi ya kusini
10.Askofu Jobu A. Mbwilo, KKKT Dayosisi ya Kusini Magharibi
11.Askofu Dk. Owdenburg M. Mdegella, KKKT Dayosisi ya Iringa
12.Askofu Renard K. Mtenji, KKKT Dayosisi ya Ulanga Kilombero
13.Askofu Dk Stephen I. Munga KKKT Dayosisi kaskazini
mashariki
14.Askofu Dk Hance Mwakabana Dayosisi ya kusini kati
15.Askofu Dk Israel-Peter Mwakyolile, KKKT Dayosisi ya Konde
16.Askofu Festo Ngowa, KKKT Dayosisi ya Dodoma
17.Askofu Jacob mameo Ole Paulo, KKKT Dayosisi ya Morogoro
18.Askofu Dk Martin F. Shayo, KKKT Dayosisi ya Kaskazini
19.Askofu Eliuphoo Y. Sima, KKKT Dayosisi ya Kati
20.Msaidizi wa Asikofu Mch. Eliraha M. Mmwari KKKT Dayosisi
ya pare
DODOMA
7 Januari 2010
0 comments:
Post a Comment