W
|
atu
akali ya tisa wanasadikiwa kupoteza maisha papo hapo katika ajali iliyotokea mchana
huu katika eneno la Mbalizi, Mbeya Vijijini.
Macho ya mwandishi wa habari
hii ameshuhudia miili tisa ikiwa imeungua vibaya na kutawanyika baada ya lori
lililokuwa na mafuta linalosadikiwa ni mali ya kampuni la LAKE OIL lenye namba
za usajili T 814 BTC lililokuwa na tera ambalo namba zake ahazitambulika mara
moja kufuatia kuungua vibaya.
Mwandishi wa habari hii anasema
ajali hiyo imehusisha magari matatu, Lori lililokuwa na namba za usajili T 299
BCE lililokuwa likishuka taratibu mteremko wa Mbalizi.
Pia Hiace T 887 AHT linalofanya
safari zake Mbalizi na Mwanjelwa na Gari Ford Double Kibbin linasadikiwa
kumilikiwa na Mbunge wa Viti maalum kwa tiketi ya Chama cha Mapinduzi, Mary
Mwanjelwa ambalo namba zake hazikupatikana mara moja kutokana na kuungua
vibaya.
Shuhuda wa ajali hiyo aliyefahamika kwa jina la Sadiki Nurdin ambaye ni utingo wa
Lori lenye namba T 299 BCE amemwambia mwandishi wa habari hii kwamba lori
lilikuwa na mafuta likiwa nyuma yao aliliona likija kwa mwendo kasi hivyo alimshtua dereva wake na hivyo
kulikwepa.
Utingo huyo ameongeza kusema
walipolikwepa lilianza kula ubavu wa
gari lao na hatimaye lilikwenda na kukutana uso kwa uso na Hiace pamoja na gari
linalosadikiwa ni la Mbunge wa Viti Maalum CCM na kusababisha maafa hayo.
Mwandishi wa habari hii amesema
kwa haraka haraka waliokufa ni 9, wawili kutoka kwenye Lori ambalo limelipuka
na kusababisha maafa hayo, watu 6 kutoka kwenye basi la abiria aina ya HIACE,
mpanda baiskeli, na mwendesha bodaboda.
Mwandishi wa habari hii anasema
idadio ya majeruhi hajipata bado licha ya kwamba wamefikishwa katika hospitali
ya Ifisi Mbeya Vijijini.
Zoezi la uokoaji kwa mara ya
kwanza limefanywa na Koplo Mathias Joachim wa
Kikosi cha Jeshi la Wananchi wa Tanzania 44 KJ Mbalizi Mbeya.
Mashuhuda wa tukio hilo
wampongeza sana Koplo huyo kwani ndiye aliyeweza pekee kuingia katika moto
uliokuwa ukiwaka kwa nguvu katika ajali hiyo.
Imeandikwa
na Kupigwa picha na Charles Mwaipopo wa MALAFYALELEO, Mbeya
0 comments:
Post a Comment