Kama wale wanachama wanaowania uongozi wamekithiri hivyo kwa vitendo vya rushwa, watawezaje kuongoza nafasi za serekali kwa uadilifu wapatapo madaraka serekalini?
Katiba ndio mama wa sheria zote za nchi na ndio inayotoa mwanya aidha kwa maendeleo ya nchi au kwa mwendelezo ya umaskini maana yote hayo yanategemea sheria zilivyo na zinavyozingatiwa. Tunashukuru Mola kwamba angalau kuna nia ya kurekebisha katiba yetu ili kutupatia matumaini mapya baada ya kuishi kwa muda marefu katika mfumo wa kisheria unaotoa mwanya mkubwa wa kuzorotosha maendeleo ya umma. Na ningewaasa sana watanzania wote wanaotoa maoni yao kuhusu uundaji wa katiba mpya kuangalia pia katiba za nchi zingine ambazo zimewezesha kufanya nchi hizo zisonge mbele kimaendeleo kwa kuwapa wananchi uwezo zaidi wa kulinda maslahi ya umma kuliko hii ya sasa ambayo inawapa viongozi uwezo zaidi wa kudhalilisha wananchi wanavyotaka na kuendelea kuwafanya maskini na watumwa katika nchi yao. Tujifunze mambo ya msingi kwa nchi kutoka katiba za wenzetu. Bahati mbaya mimi siwezi kuchangia mawazo yangu ana kwa ana kwa sababu nipo nje ya nchi, kwa hiyo ningependa kutoa mawazo yangu katika gazeti hili nikitumaini kwamba wanatume wanaohusika na huo mchakato wataweza kuyaona. Mawazo yangu ni kama ifuatavyo: (1) Kwanza kabisa napendekeza kwamba ile sheria ya kusema kwamba rais akishatangazwa basi hakuna chombo chenye mamlaka ya kutengua, sheria hiyo iondolewe kabisa maana ni sheria inayotoa mwanya wa kudumisha madarakani viongozi ambao wamepita kwa njia zisizo halali. Mimi ningependekeza kwamba rais akishatangazwa basi ichukuliwe kuwa ni rais halali lakini ikigundulika wakati wowote ndani ya kipindi cha mwaka mmoja tangu atangazwe, kwamba kulikuwa na ukiukwaji wa taratibu za uchaguzi ambazo zilimwingiza madarakani kwa hila na udanganyifu basi ushindi wake utenguliwe; na chama kilichoonekana kuwa kimeshinda kihalali kikabidhiwe madaraka ya kuongoza nchi…au kama inafaa zaidi, uchaguzi urudiwe lakini chama kinachotuhumiwa kukughushi matokeo kisiruhusiwe kugombea ila kilazimishwe kulipa gharama za kesi na za uchaguzi au kifutwe kabisa.
Au
Katiba mpya ya nchi ieleze kabisa kwamba matokeo ya uchaguzi yathibitishwe kwanza na mahakama; na ikiwa yana utata, mahakama iwe na mamlaka ya kutangaza kwamba uchaguzi ulikuwa batili na uchaguzi urudiwe. Ikiwa kasoro zilizojitokeza zilisababishwa na chama kinachodaiwa kushinda basi chama hicho kiondolewe sifa ya kugombea katika uchaguzi unaorudiwa. Ikiwa kulikuwa njama zozote za uvurugaji (ubadilishaji) wa matokeo kwa manufaa ya chama fulani kinyume na matokeo halisi, basi wote waliousika na vitendo hivyo hadi kupelekea kubatilishwa kwa uchaguzi washtakiwe katika mahakama ya kimataifa maana hao ni watu hatari kwa amani ya nchi.
(2) Tume ya uchaguzi iwe na wajumbe kutoka makundi mbalimbali ya kijamii na sio wanasiasa kutoka chama kimoja tu. Na tume hiyo uiundwe kwa utaratibu wa kupigiwa kura na kupitishwa na Bunge la Jamnhuri ya Muungano maana ni tume nyeti sana kwa mstakabali wa nchi.
Tume kama tuliyo nayo haiwezi kutangaza matokeo yaliyotokana na kura za wananchi maana haikuundwa kufanya hivyo: imeunda kutangaza matokeo watakayopewa na chama kilichoiunda. Hatuhitaji tume ya namna hiyo wala hatuna haja nayo. Tunahitaji tume ya kweli ya uchaguzi itakayotoa matokeo ya uchaguzi uliofanywa na wananchi na sio matokeo yaliyotengenezwa na chama.
(1) Mfumo wa uchaguzi unaopima ushindi kwa kupata zaidi ya asilimia hamsini urudishwe. Huu ndio mfumo unaothibitisha kukubalika kwa mgombea kwa walio wengi. Utaratibu wa sasa wa kushinda kwa kuangalia tu kuzidiana kwa kura hata moja haithibitishi kukubaliwa na wengi kwa mgombea. Ikiwa mgombea ameshinda kwa wingi wa kura lakini hajafikia zaidi ya asilimia hamsini basi alazimike kuunda serekali ya umoja wa kitaifa ambapo Waziri mkuu awe anatoka katika chama kilichofuata kwa wingi wa kura na awe anawajibika moja kwa moja kwa wananchi. Ikibidi makamu wa rais aongoze shughuli za serekali bungeni.
(2) Ibara ya 46 irekebishwe maana inampa rais madaraka makubwa mno ambapo hata akitenda maovu makubwa akiwa madarakani, mchakato wa kumchukulia hatua unachukua mlolongo mrefu mno na pengine isiwezekane. Ni ajabu kwamba hata kama aliwahi kuwa jambazi lililopora mali za watu na kuuwa kabla hajawa rais hawezi tena kushtakiwa awapo madarakani. Ibara hiyo inamfanya awe juu ya sheria, hivyo sio haki. Rais sio mungu-mtu.
Hapa napendekeza kwamba katiba iweke wazi kwamba rais awapo madarakani aweza kufunguliwa mashtaka wakati wowote kutokana na kosa lolote la jinai. Kama nchi zingine kama Marekani wanaweza kumuwajibisha rais wao angali madarakani ni nini kinachotuzuia sisi kuiga mambo kama hayo ambayo yana manufaa makubwa kwa umma?
(1) Mikataba ya madini na ile ya uwekezaji mwingine mkubwa uthibitishwe na Bunge la jamhuri ya Muungano badala ya mtindo wa sasa ambapo mawaziri wachache wabinafsi wanaweza kutia saini kwa maslahi yao binafsi.
(2) Kama Serekali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania haina dini, na Zanzibar ni sehemu ya Jamhuri ya Muungano, basi katiba ya Jamhuri ya Muungano iweke wazi kwamba nafasi mbalimbali za uongozi huko Zanzibar hazitashikwa kwa misingi ya ubaguzi wa kidini. Nasema hivyo kwa sababu mpaka sasa ukiangalia baraza la wawakilishi, baraza la mawaziri, wakuu wa mikoa, wakuu wa wilaya na viongozi wa ngazi mbalimbali za kisiasa na utendaji katika ngazi za juu za serekali kule Zanzibar, sijui wakristu ni wangapi kati ya hao!!! Vinginevyo katiba iseme pia wazi kwamba Zanzibar ni nchi ya kiislamu na kwa hiyo viongozi watakuwa waislamu tu.
(3) Katiba mpya iruhusu mgombea binafsi kwa ngazi ya urais. Hii ni muhimu kwa sababu ataangalia mafaa ya Umma kuliko ilivyo sasa ambapo wagombea huangalia mafaa ya vyama vyao. Akichaguliwa basi aunde serekali ya umoja wa Kitaifa kwa kuhusisha vyama vyote vyenye wajumbe wengi katika bunge la Jamhuri ya Muungano na baraza la wawakilishi.
(1) Majaji wasiteuliwe moja kwa moja na rais. Hawa ni watu muhimu mno kwa mstakabali wa nchi. Kila jaji apigiwe kura ya kukubaliwa au kukataliwa na bunge kwa misingi ya sifa alizo nazo za kielimu na pia uadilifu wa kazi na hasa utendaji wake wa kusimamia haki. Pia Bunge liwe na uwezo wa kupiga kura ya kumwondoa jaji katika utumishi ikiwa itaonekana kwamba utendaji wake una mashaka makubwa kuhusu usimamizi wa haki.
(2) Mkurugenzi wa TAKUKURU asiwajibike kwa rais.
(3) Ardhi ni mali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania. Bunge liwe na mamlaka kuhusu ardhi ambayo ni mali ya wananchi kwa ujumla na sio mali ya rais. Kwa sasa kuna hatari kwamba rais peke yake aweza kuamua kuuza ardhi maana ni yake!! Hatari hiyo ipo pia pale mtu binafsi anapojisikia pia kwamba ardhi ni yake na hakuna chombo chochote au mamlaka yoyote inayoweza kumwondoa katika ardhi hiyo hata kwa manufaa ya umma .
(4) Iwekwe wazi kwamba polisi hawana mamlaka ya kumpiga au kumwadhibu kwa namna yoyote mtuhumiwa ambaye ameshakamatwa na yuko chini ya ulinzi. Ikibainika, serekali ifunguliwe mashataka pamoja na polisi aliyehusika ili fidia ya haki itolewe.
(5) Katiba iweke wazi kwamba hakuna msamaha wa kodi kwa muwekezaji yoyote awe wa ndani au wa nje. Mtu akishaamua kufanya biashara basi alipe kodi ya asilimia iliyowekwa kuendana na kiasi cha mapato yake.
(6) Wafanyakazi wote walioajiriwa na serekali na katika makampuni ya kibiashara walipiwe bima ya afya na waajiri wao.
(7) Katiba mpya iweke wazi kwamba wanawake wana haki sawa na wanaume ya kuthaminiwa utu na haki. Hivyo, ubaguzi dhidi ya wanawake kwa misingi ya kijinsia kama kuwanyima haki ya kumilikishwa sehemu ya mali ya familia kama ilivyo wanaume, kuwanyima haki ya elimu, haki ya kuwa huru kuendesha maisha yao ni kosa la jinai. Na kwa kuwa tatizo la unyanyasji wa kijinsia katika familia ni kubwa sana basi katiba iseme wazi kwamba ni kosa la jinai kwa mwanafamilia yoyote kumnyanyasa mwingine kwa misingi ya kijinsia.
Kama wale wanachama wanaowania uongozi wamekithiri hivyo kwa vitendo vya rushwa, watawezaje kuongoza nafasi za serekali kwa uadilifu wapatapo madaraka serekalini?
ReplyDelete
ReplyDeleteMaoni yangu kuhusu Katiba Mpya
Katiba ndio mama wa sheria zote za nchi na ndio inayotoa mwanya aidha kwa maendeleo ya nchi au kwa mwendelezo ya umaskini maana yote hayo yanategemea sheria zilivyo na zinavyozingatiwa.
Tunashukuru Mola kwamba angalau kuna nia ya kurekebisha katiba yetu ili kutupatia matumaini mapya baada ya kuishi kwa muda marefu katika mfumo wa kisheria unaotoa mwanya mkubwa wa kuzorotosha maendeleo ya umma.
Na ningewaasa sana watanzania wote wanaotoa maoni yao kuhusu uundaji wa katiba mpya kuangalia pia katiba za nchi zingine ambazo zimewezesha kufanya nchi hizo zisonge mbele kimaendeleo kwa kuwapa wananchi uwezo zaidi wa kulinda maslahi ya umma kuliko hii ya sasa ambayo inawapa viongozi uwezo zaidi wa kudhalilisha wananchi wanavyotaka na kuendelea kuwafanya maskini na watumwa katika nchi yao. Tujifunze mambo ya msingi kwa nchi kutoka katiba za wenzetu.
Bahati mbaya mimi siwezi kuchangia mawazo yangu ana kwa ana kwa sababu nipo nje ya nchi, kwa hiyo ningependa kutoa mawazo yangu katika gazeti hili nikitumaini kwamba wanatume wanaohusika na huo mchakato wataweza kuyaona. Mawazo yangu ni kama ifuatavyo:
(1) Kwanza kabisa napendekeza kwamba ile sheria ya kusema kwamba rais akishatangazwa basi hakuna chombo chenye mamlaka ya kutengua, sheria hiyo iondolewe kabisa maana ni sheria inayotoa mwanya wa kudumisha madarakani viongozi ambao wamepita kwa njia zisizo halali. Mimi ningependekeza kwamba rais akishatangazwa basi ichukuliwe kuwa ni rais halali lakini ikigundulika wakati wowote ndani ya kipindi cha mwaka mmoja tangu atangazwe, kwamba kulikuwa na ukiukwaji wa taratibu za uchaguzi ambazo zilimwingiza madarakani kwa hila na udanganyifu basi ushindi wake utenguliwe; na chama kilichoonekana kuwa kimeshinda kihalali kikabidhiwe madaraka ya kuongoza nchi…au kama inafaa zaidi, uchaguzi urudiwe lakini chama kinachotuhumiwa kukughushi matokeo kisiruhusiwe kugombea ila kilazimishwe kulipa gharama za kesi na za uchaguzi au kifutwe kabisa.
Au
Katiba mpya ya nchi ieleze kabisa kwamba matokeo ya uchaguzi yathibitishwe kwanza na mahakama; na ikiwa yana utata, mahakama iwe na mamlaka ya kutangaza kwamba uchaguzi ulikuwa batili na uchaguzi urudiwe. Ikiwa kasoro zilizojitokeza zilisababishwa na chama kinachodaiwa kushinda basi chama hicho kiondolewe sifa ya kugombea katika uchaguzi unaorudiwa. Ikiwa kulikuwa njama zozote za uvurugaji (ubadilishaji) wa matokeo kwa manufaa ya chama fulani kinyume na matokeo halisi, basi wote waliousika na vitendo hivyo hadi kupelekea kubatilishwa kwa uchaguzi washtakiwe katika mahakama ya kimataifa maana hao ni watu hatari kwa amani ya nchi.
(2) Tume ya uchaguzi iwe na wajumbe kutoka makundi mbalimbali ya kijamii na sio wanasiasa kutoka chama kimoja tu. Na tume hiyo uiundwe kwa utaratibu wa kupigiwa kura na kupitishwa na Bunge la Jamnhuri ya Muungano maana ni tume nyeti sana kwa mstakabali wa nchi.
Tume kama tuliyo nayo haiwezi kutangaza matokeo yaliyotokana na kura za wananchi maana haikuundwa kufanya hivyo: imeunda kutangaza matokeo watakayopewa na chama kilichoiunda. Hatuhitaji tume ya namna hiyo wala hatuna haja nayo. Tunahitaji tume ya kweli ya uchaguzi itakayotoa matokeo ya uchaguzi uliofanywa na wananchi na sio matokeo yaliyotengenezwa na chama.
Maoni yangu kuhusu Katiba Mpya
ReplyDelete(1) Mfumo wa uchaguzi unaopima ushindi kwa kupata zaidi ya asilimia hamsini urudishwe. Huu ndio mfumo unaothibitisha kukubalika kwa mgombea kwa walio wengi. Utaratibu wa sasa wa kushinda kwa kuangalia tu kuzidiana kwa kura hata moja haithibitishi kukubaliwa na wengi kwa mgombea. Ikiwa mgombea ameshinda kwa wingi wa kura lakini hajafikia zaidi ya asilimia hamsini basi alazimike kuunda serekali ya umoja wa kitaifa ambapo Waziri mkuu awe anatoka katika chama kilichofuata kwa wingi wa kura na awe anawajibika moja kwa moja kwa wananchi. Ikibidi makamu wa rais aongoze shughuli za serekali bungeni.
(2) Ibara ya 46 irekebishwe maana inampa rais madaraka makubwa mno ambapo hata akitenda maovu makubwa akiwa madarakani, mchakato wa kumchukulia hatua unachukua mlolongo mrefu mno na pengine isiwezekane. Ni ajabu kwamba hata kama aliwahi kuwa jambazi lililopora mali za watu na kuuwa kabla hajawa rais hawezi tena kushtakiwa awapo madarakani. Ibara hiyo inamfanya awe juu ya sheria, hivyo sio haki. Rais sio mungu-mtu.
Hapa napendekeza kwamba katiba iweke wazi kwamba rais awapo madarakani aweza kufunguliwa mashtaka wakati wowote kutokana na kosa lolote la jinai. Kama nchi zingine kama Marekani wanaweza kumuwajibisha rais wao angali madarakani ni nini kinachotuzuia sisi kuiga mambo kama hayo ambayo yana manufaa makubwa kwa umma?
Maoni yangu kuhusu Katiba Mpya
ReplyDelete(1) Mikataba ya madini na ile ya uwekezaji mwingine mkubwa uthibitishwe na Bunge la jamhuri ya Muungano badala ya mtindo wa sasa ambapo mawaziri wachache wabinafsi wanaweza kutia saini kwa maslahi yao binafsi.
(2) Kama Serekali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania haina dini, na Zanzibar ni sehemu ya Jamhuri ya Muungano, basi katiba ya Jamhuri ya Muungano iweke wazi kwamba nafasi mbalimbali za uongozi huko Zanzibar hazitashikwa kwa misingi ya ubaguzi wa kidini. Nasema hivyo kwa sababu mpaka sasa ukiangalia baraza la wawakilishi, baraza la mawaziri, wakuu wa mikoa, wakuu wa wilaya na viongozi wa ngazi mbalimbali za kisiasa na utendaji katika ngazi za juu za serekali kule Zanzibar, sijui wakristu ni wangapi kati ya hao!!! Vinginevyo katiba iseme pia wazi kwamba Zanzibar ni nchi ya kiislamu na kwa hiyo viongozi watakuwa waislamu tu.
(3) Katiba mpya iruhusu mgombea binafsi kwa ngazi ya urais. Hii ni muhimu kwa sababu ataangalia mafaa ya Umma kuliko ilivyo sasa ambapo wagombea huangalia mafaa ya vyama vyao. Akichaguliwa basi aunde serekali ya umoja wa Kitaifa kwa kuhusisha vyama vyote vyenye wajumbe wengi katika bunge la Jamhuri ya Muungano na baraza la wawakilishi.
Maoni yangu kuhusu Katiba Mpya
ReplyDelete(1) Majaji wasiteuliwe moja kwa moja na rais. Hawa ni watu muhimu mno kwa mstakabali wa nchi. Kila jaji apigiwe kura ya kukubaliwa au kukataliwa na bunge kwa misingi ya sifa alizo nazo za kielimu na pia uadilifu wa kazi na hasa utendaji wake wa kusimamia haki. Pia Bunge liwe na uwezo wa kupiga kura ya kumwondoa jaji katika utumishi ikiwa itaonekana kwamba utendaji wake una mashaka makubwa kuhusu usimamizi wa haki.