Pages

Ads 468x60px

Monday, October 22, 2012

MKUU WA MKOA WA MBEYA AZINDUA MAONYESHO YA TASISI YA TAIFA YA TAFITI ZA MAGONJWA MBALIMBALI YA BINADAMJU (NIMR) MKOANI HAPA


ABASI KANDOLO amepongeza sana maonyesho hayo ya siku moja yaliyohudhuliwa na viongozi  wananchi mbalimbali kwa lengo la kuhamasisha kupima afya zao na kuharakisha maendeleo ya kaya na kwa taifa zima la Tanzania

KANDOLO  amesema maonyesho hayo yatasaidia kuwapatia elimu wananchi  wa mkoa wa mbeya kujua umuhimu wa kufika hospitalini mapema na kuachana na kasumba ya kwenda kwa wagana wa kienyeji ambao hupelekea kuchelewa kujua afya ya mgojwa mapema

Pia amewataka wananchi kuacha tabia ya kunywa dawa kienyeji bila kupata vipimo kutoka kwa madaktari kitu ambacho huperekea tafiti mbalimbli kukosa tiba sahihi kutokana na usugu kwa  magojwa kuzizoea dawa

Kwa upane wa waganga wa kienyeji amewataka kutumia fursa hii ya kuleta dawa zao katika maabara hii ili zipimwe na na kuwekwa katika vifungashio vilivyo bora na kuongeza thamani ya dawa hizo badara ya kuweka matambala barabarani ili kujitangaza.

Naye mkurugenzi wa Taasisi ya Taifaya ya tafiti za magonjwa ya binadamu NIMR  Dr mwele Malecela amewapongeza wananchi wa mkoa wa mbeya kwa kujitikeza kwa wingi katika maonyesho hayo kwani yametia fola japokuwa ni kwa mara ya kwanza kufanyika mkoani hapa
  
Viongozi waliohudhuria maonyesho hayo ni pamoja na mkurugenzi wa Taifa wa taasisi hiyo Dr Mwele Malecela, Kaimu mkurugenzi wa NIMR Tukuyu Gibson Kagaruki na Murugenzi wa kituo cha NIMRI Mbeya Dr Leonard Maboko

Mwisho Dr  Leonard Maboko mkurugenzi wa kituo cha NIMR Mbeya amewataka wakazi wa mkoa wa huua kujivunia kituo hiki na kukifanya ni cha kwao hivyo wafike na kupima afya zao 
 MKUU WA MKOA WA MBEYA ABASI KANDOLO AKITEMBELEA MABANDA MBALIMBALI ILI KUJIONEA SHUNGHURI ZA TAFITI NAUPIMAJI ZINAVYOFANYWA

0 comments:

Post a Comment