Pages

Ads 468x60px

Thursday, January 3, 2013

ASKOFU KIONGOZI WA KANISA LA MORAVIANI TANZANIA ALINIKISA CHEYO AMEWATAKA WAUMINI WA KRISTO NCHINI KUWA WAAMINIFU


 PIA KUTOSHEKA NA MISHAHARA YAO KATIKA KUTENDA KAZI WALIZOPEWA KAMA DHAMANA NA MUNGU KWA WENGINE

Hayo ameyasema katika ibaada ya kuukaribisha mwaka mpya iliyofanyika katika kanisa la moraviani ushirika wa mbeya mjini CHEYO amewataka watu wanaotaka kupewa huduma na wao kuwahurumia kwani wamepewa kama dhamana na mungu,


Aidha amewasihi kutosheka na mishahara yao wanayoipata kiharali ili kuondokana na taifa kushamili kwa wimbi hili la rushwa kwani wanaoweza kukomsha ni wakristo kwakuwa wao wana dhamana ya kumtangaza YESU KRISTO, hivyo wawe ni kielelezo kwa jamjii inayo wazunguka

Cheyo amesema ni lazima muumini wa kweli awe ni mkarimu kwa wengine kwakuwa mungu mwenyewe ndiye chanzo cha ukarimu huo kwa wanadamu hivyo kwa mwaka huu mpya tuanze kwa kuonyeshwa matunda hayo ya ukristo wetu kwa matendo yanayoonekana kwa macho.

Aliongeza kua kila muumni wa kristo kuacha kujitetea pindi unapochafuliwa kwa maneno na watu kwa j
ambo ambalo hujalitenda kwani yupo mtetezi wetu YESU kwa kufanya hivyo unaweza kuwapa watu faida na kujichafua zaidi, Pia kwa wale wenye tabia za kusema uongo na uchezi kwa wengine kuacha mara moja kwani hiyo ni kazi ya shetani


ASKOFU KIONGOZI ALINIKISA ZHEYO AKIONGEA NA WAUMINI WA KANISA LA MORAVIANI USHIRIKA WA MBEYA MJINI


 WAKRISTO WA KANISA LA MORAVIANI USHIRIKA WA MBEYA MJINI WAKIMSIKILIZA KWA MAKINI ASKOFU CHEYO


KWAYA YA VIJANA (A) USHIRIKA WA MBEYA MJINI WAKIIMBA WIMBO MAARUMU KATIKA IBAADA YA KUUARIBISHA MWAKA MPYA

0 comments:

Post a Comment