NI KATIKA IBAADA MAARUMU ILIYOFANYIKA KATIKA KANISA LA
MORAVIANI USHIRIKA WA RUANDA
Mbunge wa viti maalumu jijini mbeya MARY MWANJELWA amemwaga
machozi ya uchungu kumshukuru mungu kwa kumuokoa na ajari mbaya iliyo kuwa
imetokea October 2 mwaka jana maeneo ya mbalizi mbeya vijijini iliyoghalimu uhai
wamaisha ya watu zaidi ya kumi na moja.
Tukio hilo limetokea katika ibaada iliyoandaliwa maalumu
kumshukuru mungu iliyofanyika katika kanisa la moraviani ushirika wa RUANDA
kisha kuhudhuliwa na viongozi mbalimbali wa serikali na kidini akiwemo baba
Askofu kiongozi wa kanisa la Moraviani Tanzania ALINIKISA CHEYO.
Wengine ni Naibu Waziri wa elimu na ufundi PHILP MULUGO
mkurugenzi wa shirika la nyumba MANYAMA mwenyekiti wa vijana uvccm AMANI KAJUNA
pamoja na madiwani wa kata mbalimbali.
Katika ibaada hiyo MARY pamoja na familia yake walitoa shukurani
yao ya pekee pesa ambazo hazikitajwa
kiasi gani, pia alitoa msaada wa baiskeli kumi kwa wenye ulemavu wa viungo
MARY ameshukuru sana mungu kumtoa katika ajali ambayo
wengine walopoteza maisha yao akiwemo katibu wake ambaye aliteketea papo hapo kwa
moto, Amewataka waumini na wanachi wote kuiombea amani inchi yetu na mkoa wa
mbeya ili kuondokana na machafukao yanayo tokea kila wakati pasipo na sababu.
Aidha kwaupande wake Naibu waziri elimu na ufundi PHILP
MULUGO amempongeza MARY MWANJELWA kwakumkumbuka mungu kuwa ndiye aliye mponya
na ajari hiyo na kisha kumshuru, Amewataka waumini kujifunza mfano huo na kutomuacha mungu kwani ndiye muweza wa mambo
yote.
Naye Askofu kiongozi wa kanisa la moraviani Tanzania ALIKISA
CHEYO amesema tendo alilotenda hapa ni jema tena amemuheshimu sana mungu na
hata kwa wana jimii nzima kwa kuwakumbuka watu wasio jiweza na wenye ulemavu
kwakutoa nyenzo itakayo warahisishia kutembea.
Ameongeza kuwa hakuwasaidia walemavu tu bali ni kwa wana
MBEYA wote kwa tendo hili tutamkumbuka katika maisha yetu yote na mungu
aendelee kumzidishia Baraka tele.
0 comments:
Post a Comment