Taarifa
kutoka ofisi ya Papa imesema kuwa, hatua hiyo imetokana na kuendelea kudhoofika
afya ya kiongozi huyo wa kidini. Papa Benedict XVI mwenye umri wa miaka 85
alichaguliwa kuliongoza Kanisa Katoliki Aprili 19 mwaka 2005 baada ya kufariki
dunia Papa John Paul II.
Ingawa
Vatican imesema sababu ya kutaka kujiuzulu kiongozi huyo ni umri wake mkubwa,
weledi wa mambo wanaamini kwamba kashfa mbalimbali zilizokumba kanisa hilo chini
ya uongozi wake ni miongoni mwa sababu za yeye kuchukua uamuzi huo. Papa
Benedict XVI anakuwa kiongozi wa pili wa kanisa katoliki kujiuzulu. Mwaka 1296,
Celestine V alijiuzulu kutokana na sababu za kiafya.
0 comments:
Post a Comment