Baba
Mtakatifu Francis, leo ametawazwa rasmi kuliongoza Kanisa Katoliki duniani
katika Ibada ya Misa inayofanyika kwenye Uwanja wa Mtakatifu Petro mjini
Vatican.
Katika Ibada hiyo, Baba
Mtakatifu Francis amevalishwa pete ikiashiria sasa amekuwa Baba Mtakatifu wa
266. Ibada hiyo inahudhuriwa na waumini wengi, tangu Mei, mwaka 2011 ambapo
zaidi ya watu milioni 1.5 walifika Vatican kuhudhuria sherehe za kutangazwa
mwenye heri, Papa Yohana Paulo wa Pili . Viongozi 130 kutoka duniani kote,
wanahudhuria Ibada hiyo, akiwemo Makamu wa Rais wa Marekani, Joe Biden na Rais
wa Zimbabwe, Robert Mugabe.
0 comments:
Post a Comment