Hii ndiyo ofisi inayotumika kuwatesa wanafunzi ofisi hii huitwa guantanamo bay camp
IKIWA zimepita siku chache tangu Taasisi ya
kuzuia na kupambana na Rushwa (TAKUKURU) Mkoa wa Mbeya kuwakamata Walimu wawili
wa Shule ya Sekondari ya Forest wakituhumiwa kupokea rushwa sakata hilo
limechukua sura mpya baada ya wanafunzi wa shule hiyo kuandamana.
Maandamano ya wanafunzi hao yametokana na Walimu
hao kuwa nje ya dhamana na kuendelea kufundisha katika shule hiyo jambo ambalo
wanafunzi hao wamelipinga na kusababisha maandamano yaliyozuiliwa na jeshi la
polisi walipokuwa wakitaka kuelekea kwenye Ofisi za Ofisa Elimu wa Mkoa.
Kutokana na hali hiyo Ofisa Elimu wa Mkoa wa
Mbeya Juma Kaponda amelazimika kufika Shuleni hapo kisha kuzungumza na
wanafunzi ambao walimtajia sababu zaidi ya kumi zilizosababisha kufanya
maandamano hayo.
Wamezitaja sababu hizo kuwa ni pamoja na sakata
la walimu waliokamatwa kwa rushwa kuachiwa na kuendelea kufundisha, Walimu
kutofundisha, Vitisho vya walimu kwa wanafunzi, Wazazi kutukanwa na walimu,
Kutokuwa na imani na Mkuu wa Shule pamoja na ujirani wa walimu watuhumiwa na
mkuu wa Shule.
Wamezitaja sababu zingine kuwa ni Mkuu wa shule
kutumia matofali ya shule kujengea madarasa badala ya wigo,kutokuwa na vifaa
vya michezo pamoja na kutotolewa kwa vibali vya kwenda kucheza na shule jirani.
Wameongeza kuwa Shule haifanyi mikutano ya
wanafunzi( baraza la shule la wanafunzi), kutokuwa na vitambulisho vya
wanafunzi, michango ya wigo, michango ya wigo wa shule na michango ya masomo ya
jioni.
Akijibu tuhuma hizo Ofisa Elimu wa Mkoa wa Mbeya
Juma Kaponda amesema suala la walimu hao kukamatwa na kufikishwa Takukuru ni
suala la ngazi nyingine hivyo hawatakiwi kulizungumzia.
Kuhusu madai ya walimu kutofundisha Kaponda
amesema si sababu ya kweli kutokana na wanafunzi hao kuwa kwenye mitihani ya
kufungia mhura hivyo walimu hawawezi kuingia madarasani kufundisha.
Pia amewaagiza walimu hao kuwa na ushirikiano na
wanafunzi na kutotoa lugha za vitisho kwa wanafunzi ambapo pia aliwaagiza
wanafunzi kuwa watulivu na kuwasikiliza walimu wao.
Aidha amewaagiza walimu haokutoitisha mikutano
ya wazazi pasipo kuwepo kwa bodi ya shule ambapo ameagiza kuwa kila mkutano wa
wazazi utaklapofanyika ni vema mwenyekitiwa bodi ( ya shule akaongoza mikutano
hiyo.
Kuhusu suala la vibali vya michezo, mikutano ya
baraza la wanafunzi na vitambulisho Ofisa huyo aliagiza Mkuu wa Shule
hiyo Cesilia Kakera kulishughulikia mara moja na kumpelekea taarifa ofisini
kwake mara moja.
Kamanda wa Takukuru Mkoa wa Mbeya Daniel Mtuka
alipoulizwa suala la walimu hao kuendelea na kazi ili hali walikuwa wamekamatwa
kwa tuhuma za rushwa Kamanda huyo alisema wameachiwa kwa dhamana.
Mtuka amesema baada ya watuhumiwa hao ambao
walikamatwa Machi 4, Mwaka huu bado wanashikiliwa na kikosi chake ingawa wako
nje kwa dhamana na kuongeza kuwa uchunguzi wa kesi hiyo bado haujakamilika
hivyo hawawezi kuwazuia kuendelea na kazi.
Amesema baada ya kukamilika uchunguzi ndipo
itakapojulikana ni hatua ipi itakayofaa kuchukuliwa dhidi ya watuhumiwa kama
watakuwa wamebainika kuhusika na sakata hilo.
Walimu
hao walikamatwa kwa tuhuma za kushawishi na kupokea rushwa ya kati ya shilingi
500 na 1,000 kutoka kwa wanafunzi wanaochelewa kufika shuleni asubuhi kila
siku.
Kamanda
wa Takukuru Mkoa wa Mbeya Daniel Mtuka, alisema walimu hao walikamatwa baada ya
kupokea taarifa kutoka kwa baadhi ya wanafunzi wa shule hiyo baada ya kuchoshwa
na tabia hiyo.
Mtuka
amewataja walimu hao kuwa ni Solomoni Mwasote na Faustin Robert ambao
walikamatwa shuleni hapo wakiwa wanaendelea na zoezi hilo la kuwalipisha
wanafunzi fedha.
HABARI NA J. MWAISANGO
|
0 comments:
Post a Comment