Huenda Rais Uhuru Kenyatta akalitangaza Baraza la Baraza la mawaziri wiki hii.
Nairobi.Baraza
la mawaziri nchini Kenya linangojewa kwa hamu na wananchi ambapo wangi
wanatarajia liwe la mseto kama ilivyo Katiba ya Kenya.
Taarifa kutoka Kenya ambazo ni za kuaminika
zimesema kwamba kuna uwezekano mkubwa kutangazwa kwa Baraza hilo kati
kati ya wiki hii.
Pia Taarifa zilifichua kwamba washirika kwenye
muungano wa Jubilee bado wanajadiliana kuhusu ni upande upi utatoa
nafasi kwa baadhi ya vyama vidogo vilivyotia sahihi mkataba wa maelewano
baada ya uchaguzi mkuu kwa lengo la kuimarisha utawala wa Jubielee.
Kutokana na hali hiyo raia wa Kenya wamekuwa wakisubiri kwa hamu kusikia baraza jipya la mawaziri likitangazwa .
Taarifa ziliendeela kudodosa kwamba mahojiano na
washirika wa karibu wa viongozi yalionyesha kuwa viongozi hao wameamua
kubadilisha kabisa muundo wa utawala.
Kwa sasa anachokifanya rais wa Kenya Uhuru
Kenyatta akiwa na timu yake ,anaandaa majina ya baraza lake la Mawaziri
na pia makatibu,wakuu wa mashirika pamoja na nyadhifa zingine za juu
wakiwemo wakurugenzi wa Wizara na Idara.
Hiyo ina maana kuwa Wakenya watajionea baraza
jipya kabisa la mawaziri, makatibu wapya, mabalozi, maofisa wakuu wa
mashirika ya serikali na wakurugenzi wa wizara na idara mbalimbali.
Hata hivyo awali Rais Kenyatta alishatoa ahadi ya
kulitangaza baraza lake la mawaziri wapya huku akizingatia taaluma,
utendaji wa kazi, uwakilishi wa kimaeneo na jinsia.
Kutokana na hali hii, baadhi ya mabalozi walioagizwa warejee nyumbani huenda wasirudi katika nafasi zao za awali.
0 comments:
Post a Comment