NAIROBI, Kenya
Rais Uhuru Kenyata ametangaza siku tatu za maaombolezo kufuatia tukio la Ugaidi lililofanywa na wanamgambo wa Al Shabaab.
Jumla
ya watu 72 wameuawa katika tukio hilo huku wanajeshi sita wa Kenya
wakiwa wamepoteza maisha wakati walipokuwa wakijaribu kuokoa maisha ya
watu anaoshikiliwa mateka na magaidi wa al Shabab katika jumba lenye
maduka la Wastgate jijini Nairobi.
Askari wengine 8 wanaripotiwa kuwa mahututi baada ya kujeruhiwa katika mapambano hayo yanayoendelea hadi sasa.
Hayo yamesemwa na Mkuu wa Jeshi la Ulinzi la Kenya (KDF) Jenerali Julius Karangi.
Duru
za Kenya zinaripoti kuwa hadi sasa watu 72 wakiwemo raia sita wa nchi
za nje wamethibitishwa kuwa wameuawa pamoja na magaidi kadhaa
wamekamatwa na wanahojiwa vyombo vya ulinzi na usalama kuhusiana na
tukio hilo katika jengo la maduka la Westgate nchini Kenya.
Wakati
huo huo Waziri wa Mambo ya Nje wa Kenya Balozi Amina Mohammed amesema
kuwa Wamarekani wawili au watatu na Mwingereza mmoja wamehusika katika
shambulizi lililofanywa na magaidi dhidi ya jumba la maduka la Westgate
jijini Nairobi.
Balozi
Amina Mohammed amesema washambuliaji hao walikuwa wakishirikiana na
wenzao katika maeneo mbalimbali ya dunia kwa ajili ya kuua watu mwishoni
mwa wiki mjini Nairobi. Waziri wa Mambo ya Nje wa Kenya amesisitiza
kuwa shambulizi la sasa mjini Nairobi limefanyika kitaalamu.
Jengo la Maduka la Westgate
Baadhi ya watu waliookolewa kutoka katika jengo la Westgate.
Wanamgambo wa Al Shabaab
0 comments:
Post a Comment