WATU nane wamefariki
katika matukio matatu ya usalama barabarani mkoani Mbeya.
Kwa mujibu wa taarifa
ya kamanda wa polisi mkoa wa Mbeya Diwani Athumani, imesema kuwa MNAMO TAREHE 22.09.2013 MAJIRA YA SAA 20:00HRS HUKO SOKOMATOLA BARABARA YA
SOKOMATOLA/STENDI KUU JIJI NA MKOA
WA MBEYA.
GARI T.223 AGQ AINA YA TOYOTA HIACE LIKIENDESHWA NA DUNIA S/O FRANSIS, MIAKA 38, MNGONI, MKAZI WA AIR PORT LILIACHA
NJIA KISHA KUPINDUKA NA KUSABABISHA VIFO
VYA ABIRIA SITA, KATI YAO WANAUME WANNE NA WANAWAKE WAWILI
AMBAO BADO HAWAJAFAHAMIKA MAJINA WALA ANUANI ZAO.
AIDHA
KATIKA AJALI HIYO WATU SABA
WALIJERUHIWA AMBAO NI 1. JUMA S/O WARIOBA, MIAKA 32, MKAZI WA
SAE 2. MWANDELA S/O MWAMSI, MIAKA
22, MKAZI WA MAJENGO 3. KAMBI S/O ALLY,
MIAKA 32, MKAZI WA IRINGA 4. SELEMAN S/O
SHELUKINDO, MIAKA 25, MSAMBAA, MKAZI WA ILEJE 5.NURU S/O SHELUKINDO, MIAKA 32, MSAMBAA, MKAZI WA ILEJE 6. BAHATI D/O ALLY, MIAKA 14, MKAZI WA
SONGEA NA 7. DUNIA S/O FRANSIS AMBAO
WOTE WAMELAZWA HOSPITALI YA RUFAA MBEYA.
CHANZO KINAENDELEA
KUCHUNGUZWA JAPO TAARIFA ZA AWALI ZINAONYESHA KUWEPO KWA HITILAFU KWENYE BREAK.. MIILI YA MAREHEMU IMEHIFADHIWA HOSPITALI YA
RUFAA MBEYA. DEREVA AMEKAMATWA, NA ANAENDELEA KUHOJIWA.
KAMANDA
WA POLISI MKOA WA MBEYA KAMISHNA MSAIDIZI WA POLISI DIWANI ATHUMANI ANATOA WITO KWA MADEREVA KUWA MAKINI
WANAPOTUMIA VYOMBO VYA MOTO KWA KUZINGATIA SHERIA ZA USALAMA BARABARANI ILI
KUEPUSHA AJALI ZINAZOWEZA KUEPUKIKA. AIDHA ANATOA RAI KWA WANANCHI KUFIKA
HOSPITALI YA RUFAA MBEYA KWA AJILI YA UTAMBUZI WA MIILI YA MAREHEMU.
0 comments:
Post a Comment