Joyce
 Banda alichaguliwa kama Rais wa kwanza mwanamke Kusini mwa Afrika April
 2012. Akawa rais wa Malawi alipomrithi mtangulizi wake aliyefariki 
kutokana na mshtuko wa moyo.
Michelle Bachelet amechaguliwa kama Rais wa Chile kwa muhula wa pili na kumshinda mpinzani wake Evelyn Matthei kwa kura nyingi.
Rais
 wa Liberia,Ellen Johnson Sirleaf, 72, alitajwa kama mmoja wa washindi 
wa tuzo ya amani ya Nobel mwaka 2011. Alichaguliwa kama Rais wa kwanza 
mwanamke barani Afrika mwaka 2005 miaka miwili baada ya kumalizika kwa 
vita vya wenyewe kwa wenyewe vya miaka 14 Liberia.
Sheikh Hasina alichaguliwa kwma waziri mkuu wa kwanza wa Bangladesh kwa muhula wa pili mwezi Januari mwaka 2009. Lakini mwaka 2008 chama chake cha Awami, kilipata ushindi mkubwa dhidi ya mpinzani wake Begum Khaleda Zia.
Korea
 Kusini imemchagua rais wake wa kwanza mwanamke Park Geun-hye, kwenye 
uchaguzi uliokuwa na ushindani mkali Disemba mwaka 2012. Babake Park 
Chung-hee alitawala nchi hiyo kwa miaka 18.
Waziri
 mkuu wa Thailand, ingluck Shinawatra dadake mdogo waziri mkuu 
aliyeondolewa mamlakani Thaksin Shinawatra, aliongoza chama chake cha 
upinzani kuweza kushinda uchaguzi uliofanyika Julai 2011.
Helle
 Thorning-Schmid alichaguliwa kama waziri mkuu wa kwanza mwanamke wa 
Denmark, baada ya chama chake kupata ushindi kwenye uchaguzi uliofanyika
 Septemba mwaka 2011. Thorming alikosolewa hivi karibuni kwa kujipiga 
picha na waziri mkuu wa Uingereza Cameron na Rais Barack Obama kwenye 
ibada maalum ya hayati Mandela.
Dalia Grybauskaite alichaguliwa kama rais wa kwanza wa Lithuania katika uchaguzi mkuu wa Mei 2009. Alishinda kwa kura 69%.  
Chansela
 wa Ujerumani, Angela Merkel anajulikana kama kiongozi asiyekuwa na mbwe
 mbwe nyingi na kusababisha watu kumuita..Mutti..mama wa taifa. Markel 
anajiandaa kwa muhula wa tatu baada ya kushinda uchaguzi wa Septemba 22.
Rais
 wa Argentina, Cristina Fernandez alishinda uchaguzi uliofanyika mwezi 
Oktoba mwaka 2007 ushindi ambao wengi walisema ulitokana na umaarufu wa 
mumewe aliyekuwa Rais Nestor Kirchner. 
Rais
 wa Brazil Dilma Rousseff alichaguliwa kama rais wa kwanza mwanamke 
nchini Brazil alipochukua hatamu za uongozi kutoka kwa Luiz Inacio Lula 
da Silva mwaka 2011. Alikuwa mkuu wa majeshi kabla ya kuteuliwa na 
kumrithi Rais De Silva.
Kiongozi
 wa upinzani nchini Jamaica, Portia Simpson-Miller alishinda uchaguzi 
uliofanyika Disemba mwaka 2011 kwa idadi kubwa ya kura. Alikuwa waziri 
mkuu wa Jamaica kabla ya kushindwa kwenye uchaguzi wa mwaka 2007.
Kamla Persad-Bissessar alichaguliwa kama waziri mkuu wa kwanza mwanamke wa Trinidad and Tobago, wakati chama chake kilishinda uchaguzi kwa idadi kubwa ya kura mwezi Mei mwaka 2010. CHANZO BBC.
0 comments:
Post a Comment