MWINJILISTI ESAU MWAMTOBE
KWAYA KUU YA KANISA LA MORAVIANI USHIRIKA WA IWAMBI AMBAO WALIKUA KIVUTIO SANA KWA UIMBAJI WAO KATIKA IBAADA HIYO |
KWAYA KUU YA USHIRIKA WA MBEYA MJINI WAKITMBUIZA KATIKA IBAADA
KWAYA YA SHULE YA JUMAPILI USHIRIKA WA MBEYA MJINI
KWAYA YA UINJILISTI USHIRIKA WA MBEYA MJINI
KWAYA YA VIJANA USHRIKA WA MBEYA MJINI WAKIONGOZA NYIMBO ZA KUABUDU ZIKIONGOZWA NA MWENYEKITI WA MICHEZO PENIELI MWAISANGO
ASILI YA JINSI YA KUONGOZA NYIMBO KWA KUPIGA MAPIGO KUTOKA KWAYA KUU IWAMBI
HABARI KAMILI
WAUMINI WA DINI YA KRISTO WAMETAKIWA KULINDA SANA AMANI
KWAKUA NDIYO THAMANI YA MAISHA YA MWANADAMU HAPA DUNIANI
Hayo yamesemwa na mwinjilisti ESAU MWAMTOBE wa kanisa la
Moraviani Tanzania Jimbo la kusini magharibi ushirika wa Mbeya mjini alipokua akihubiri
katika ibaadailiyofanyika kanisani hapo jumapili ya kwanza baada ya Pasaka, akisoma
samo kutoka yohana 20:19-31 ambalo yesu alipo fufuka aliwaombea wanafunzi wake
Amani.
Ili kuipata Amani ni lazima watu wamtegemee mungu na
kumtumikia kwa uaminifu, akinukuu maandiko kutoka katika Biblia MWAMTOBE
amesema utafuteni kwanza ufalme wa mungu
na mengine yote mtazidishiwa, watu wamekua wakitafuta Amani na furaha katika
kujilimbikizia mali kitu ambacho ni ubatili mtupu
Wakristo wamekua wakikwepa majukumu yao katika kumtumikia
mungu ili kueneza ijili yake ulimwenguni kote na kusababisha baadhi ya watu
wengine kushindwa kumjua mungu na kukosa Amani katika maisha yao na hivyo wengi watakosa
kuiona mbingu kwa kukosa la kutomtumikia.
MWAMTOBE ameongeza kua hakuna jambo la muhimu katika maisha
ya mwanadam zaidi ya Amani na ndicho kitu chenye thamani kubwa, Ameongeza kua
wapo watu wana mali na kila kitu kilichopo duniani lakini hawana furaha moyoni
mwao kutokana na kutokuwa na Amani.
0 comments:
Post a Comment