Ezekieli
king alieye hukumiwa kutumikia kifungo cha miaka saba kwa kosa la kupiga na
kujeruhi.
Mwenyekiti Wa Chadema kata ya Itiji Daniel Mwakasita akiongea na mwandishi wa habari hii
Mwenyekiti wa mtaa wa itiji Ezekiel King akiwa kizimbani baada ya kuhukumiwa
Meya wa jiji la Mbeya Atanas kapunga ( Picha na Libraly yetu)
Habari Kamili
Hayo
yamesamwa na DANIELI MWAKASITA mwanyekiti wa kata ya Itiji kupitia chama hicho katika
ofisi za wilaya ya mbeya mjini walipokua wakushughulikia rufaa ya kupinga
hukumu hiyo
MWAKASITA amemtupia lawama meya wa jiji la mbeya ATANASI
KAPUNGA kuhusika na hukumu hiyo kua haikuwa na haki na kunasiasa ndani yake
kutokana na kutokuwepo kwa mahusia mazuri kati yake na mwenyekiti huyo kutoka
na kukihama chama chake mapinduzi (ccm) kwenda chadema
Ameongeza
kua meya huyo alijitapa katika moja ya mikutano yake ya hadhara kwamba atahakikisha
mwenyekti huyo ametumia gharama yoyoe kumfunga na sasa adhima yake imetimia na
wao kama wanachama wa chadema hawako tayali kukubaliana na hukumu hiyo hivyo
wana kata rufaa na kuweka wakili wa kumtetea kiongozi wao.
Nae DOMI
MWASALEMBA mmoja wa wafuasi wa chama hicho amehoji hukumu hiyo kuwa haikua na
haki kutokana na kesi kutofuta ushahidi wa kidaktali kwamba anaedai kupigwa
anatatizo la ugojwa wa akili na kwamba alileta fujo kilabuni akapingwa na watu
wengine lakini amemtaja king kwakua ndiye aliye mpeleka Polis kisha Hospital
Awali mwenyekiti wa serikali ya Mtaa
wa Itiji Jijini Mbeya mkoani Hapa anayewakilisha (CHADEMA) Ezekiel King(52) na
mwenzake Antony Simon(53) wamehukumiwa kwenda jela miaka 7 kutokana na makosa
ya shambulio na kumdhuru mwili Nicholaus Mwakasinga(56) mkazi wa Itiji mjini
humo.
Akisoma hukumu hiyo Hakimu mkazi wa
mahakama ya Mkoa wa Mbeya Maria Batulaine, mbele ya mwendesha mashtaka wa
serikali Juliana William alisema kuwa washitakiwa kwa pamoja walimshambulia
Mwakasinga kwa kumpiga na kumjeruhi kichwani na mkononi wakati wakiwa katika
kilabu cha pombe za kienyeji kilichopo mtaa wa Itiji.
Alisema anawatia hatiani washitakiwa
hao kutoka na kuwepo kwa mashaka juu ya ushahidi wa watu watatu upande
utetezi kugongana na hivyo kuridhika na ushahidi wa mashahidi wa upande wa
mashtaka na hivyo kuwatia hatiani na kwamba hata hivyo wanayo fursa ya
kukata rufaa iwapo hawajaridhika na hukumu iliyotolewa.
0 comments:
Post a Comment