Awali leo asubuhi waendesha bodaboda
hao waliandamana baada ya mwenzao mmoja aliyefahamika kwa jina la Siza
Mwambenja kuuawa na mtu anayedaiwa kuwa alitumwa na mkewe kufanya mauaji
hayo.
Wananchi wakiandamana kufunga barabara ya Esso |
Askari wa jeshi la polisi tarafa ya sisimba akizongwa na waendesha bodaboda eneo la mafiati |
Barabara zimefungwa kwa kuwekwa mawe eneo la Esso |
KIKOSI CHA KUZUIA FUJO WAKIJAZA MAJI YA KUWASHA TAYARI KWA MAPAMBANO |
Vurugu tupu |
Gari ya Polisi iliyovunjwa kioo |
HABARI KAMILI
Chanzo cha vurugu hizo inasemekana waendesha bodaboda waliandamana baada ya mwenzao mmoja aliyefahamika kwa jina la Siza Mwambenja kuuawa na mtu anayedaiwa kuwa alitumwa na mkewe kufanya mauaji hayo.
Ilielezwa kuwa marehemu aliachana na
mkewe ambapo mke inadaiwa alimtumia watu wamdhuru mumewe kwa kile
kilichoelezwa kuwa mwanaume huyo aliamua kuachana na mkewe na kuishi
sehemu nyingine kutokana na madai kutoelewana katika ndoa yao kwa mmoja
kati yao kukosa uaminifu ndani ya ndoa.
Baada ya tukio hilo la mauaji
kutokea, inadaiwa kuwa mtuhumiwa ambaye ni mke wa marehemu alikamatwa na
polisi ndipo waendesha bodaboda walielekea katika eneo hilo na kutaka
kuchukua sheria mkononi kumnyang'anya mtuhumiwa aliyekuwa chini ya
ulinzi wa polisi ili wamuadhibu.
Kitendo hicho kilisababisha kuibuka
kwa tafrani baina ya Jeshi la Polisi na waendesha boda boda ambao
walikuwa wakihitaji kumchukua mtuhumiwa ambapo walifuatilia gari la
polisi hadi kituo cha Polisi na baadaye kufunga barabara kwa kuweka
mawe, ndipo mabomu yalipoanza kurushwa na kuibuka kwa vurugu katika
maeneo ya Mafiat, Oilcom, Magorofani na Iyela.
Akizungumza tukio hilo Mwenyekiti wa
waendesha Bodaboda Jiji la Mbeya Vicent Mwashoma alisema kuwa tukio hilo
limewachanganya sana na kwamba yeye kama kiongozi alipata taarifa za
kuibuka kwa vurugu wakati polisi wamekwisha anza kurusha mabomu.
Alisema kuwa hata hivyo Jeshi la
Polisi lilipaswa kuwasiliana na uongozi wa waendesha bodaboda ili
kufanya mazungumzo kabla ya kuchukua hatua hizo ambazo zimesababisha
madhara kwa watu wengine ambao hawakuhusika katika tukio hilo.
0 comments:
Post a Comment