TAARIFA KWA UMMA
UPOTOSHAJI UNAOTOLEWA DHIDI YA TIMU YETU KUELEKEA MCHEZO WA TAREHE
13/4/2014
Kwanza nachukua nafasi hii
kuwashukuru kwa dhati wapenzi wote wa mchezo wa mpira wa miguu na wapenzi wa
Mbeya City Fc popote pale walipo kwa kuiunga mkono timu yao muda wote wa
michezo ya ligi kuu inayoelekea ukingoni hivi sasa.Klabu inathamini nafasi ya
wapenzi na washabiki katika kujenga timu imara na yenye ushindani kama
walivyofanya kwa timu yetu.
Timu yetu ilianza ligi msimu huu
2013/2014 ikiwa na malengo ya kuchukua ubingwa au kuwa katika nafasi za juu za
ligi yetu.Hiyo ndiyo dhamila iliyokuwepo kwa viongozi,wachezaji pamoja na
benchi la ufundi.
Michezo miwili imesalia kwa timu yetu
kabla ligi kuu ya Vodacom kumalizika katika msimu huu 2013/2014.katika safari
yetu ya ligi kuu kwa mara ya kwanza msimu huu, changamoto nyingi za kiutawala
na za kimtazamo kutoka kwa wadau wote wanaohusika na mchezo wa mpira wa miguu
nchini tumezishuhudia .Changamoto hizo ni ikiwemo upangaji wa ratiba usiyokuwa
na uwiano mzuri,baadhi ya mechi kuamuliwa vibaya na waamuzi wa mchezo,wizi wa
mapato ya milangoni unaotokana na mfumo mbaya wa uuzaji wa tiketi,uadilifu
mdogo kwa baadhi ya viongozi wenye dhamana ya kusimamia mpira katika ngazi zote
n,k.
Kuelekea mchezo wetu wa tarehe
13/04/2014 dhidi ya AZAM FC kumezuka propaganda chafu na ambazo si sahihi
katika ukuzaji wa mpira hasa wa ligi ndogo kama ya Tanzania. Nachukua nafasi
hii kutoa ufafanuzi wa baadhi ya mambo ambayo yamekuwa sehemu ya propaganda hizo:
1.
Propaganda kuwa Klabu imehaidiwa kununuliwa basi na hivyo inajiandaa
kutoa ushindi kwa kwa timu ya AZAM Fc na kuwarahisishia mazingira ya Ubingwa.
Halmashauri ya jiji la Mbeya limekuwa
katika mchakato wa kutafuta na kununua basi kwa ajili ya matumizi mbalimbali ya Halmashauri ikiwemo kutumiwa na timu zake (
Netiboli na Mpira wa miguu)ambazo zote zipo ligi kuu ya michezo husika kwa
kufuata sheria ya manunuzi ya Umma. Mchakato huo ulianza tarehe 8/8/2013 halmashauri ilipotangaza nia
hiyo katika gazeti la “the guardian” la tarehe hiyo kwa
tender no.LGA/069/2013-2014/MCC/G/01
hii ni baada ya Halmashauri kutenga bajeti ya fedha za makusanyo
yake ya ndani kwa mwaka wa fedha
2012/2013 na 2013/2014 ili kukidhi haja hiyo.
Tangazo hilo halikupata mzabuni mwenye
sifa za kufanya usambazaji wa basi hilo hivyo tangazo hilo lilirudiwa tena
tarehe 12/2/2014 katika gazeti la majira kwa Tender No. LGA/069/2013-2014/MCC/G/01
(Re-advitised), Mchakato na maandalizi ya ufunguaji wa ufanyaji wa tathmini wa zabuni hiyo unaendelea
kwa mujibu wa sheria ya manunuzi ya Umma.
Pamoja na mchakato huo hapo juu,pia
klabu inaendelea na mazungumzo na wadau mbalimbali wenye nia ya kuwekeza kwa
udhamini wa bidhaa zao,moja ya maeneo ya udhamini ni pamoja na ununuzi wa basi
la wachezaji taratibu na makubaliano
haya yatakapo kamili umma wa wapenda mchezo wa mpira wa mguu utajulishwa.
Hivyo propaganda hiyo kuwa klabu
imehongwa basi si za kweli na si sahii ila zina nia ya kuidhalilisha timu yetu.
2.
Propaganda kuwa Mwalimu Juma Mwambusi kanunuliwa nyumba Maeneo ya chamazi
ili apange kikosi dhaifu siku ya mchezo tarehe 13/4/2014.
Mwalimu(Kocha) Juma Mwambusi ni
muajiliwa wa Halmashauri ya jiji la Mbeya,kwa maana hiyo ni mtumishi wa Umma.
Mwalimu Mwambusi amekuwa na timu yetu kwa muda mrefu sasa na ataendelea
kuwepo.Kumekuwepo na maneno yasiyofaa dhidi ya mwalimu wetu toka mzunguko wa
pili wa ligi kuanza,maneno haya yamekuwa na nia ya kuaribu muenendo wa timu ili
ianze kufanya vibaya lakini zaidi ya hapa yana nia ya kumdhalilisha mwalimu
wetu na taaluma ya ukocha nchini.
Mwalimu amefedheheshwa sana na taarifa hizo.
3.
Propaganda kuwa wachezaji wote wa kikosi cha kwanza wamepewa hongo
wacheze chini ya kiwango 13/4/2014.
Wachezaji ndiyo wachezaji wenye
nidhamu kubwa katika ligi ya mwaka huu ndani na nje ya uwanja muda wote,ni
waadirifu na wanajua wanataka nini.Mpira ndiyo ajira yao kama watumishi wa umma
ndani ya Halmashauri ya jiji la Mbeya.Hawajawahi na wala hawatawahi kuchukua
rushwa kwa lengo la kupanga matokeo.
Klabu yetu haisadiki katika upangaji
wa matokeo ya mchezo wa mpira wa miguu kwani tunajua fika kuwa hakutaisadia
kama klabu lakini pia kama taifa katika kuendeleza mpira wa miguu nchini.
Hitimisho,
Mchezo wa mpira wa miguu una matokeo
matatu kushinda,kushindwa na kutoka sare. Klabu inaamini kuwa timu iliyojiandaa
vizuri kama yetu inastahili kupata matokeo mazuri uwanjani.Falsafa mojawapo ya
timu yetu ni kushinda mechi kwa kucheza mpira unaovutia na kuwaburudisha
watazamaji.
Tuhuma mbalimbali za upangaji matokeo
katika ligi yetu zimeanza kuota mizizi hasa ligi inapoingia mzunguko wa pili
,katika suala hili kama ambavyo linataka kuhusishwa nasi yawezekana propaganda
hizi kwa upande wa timu zinazotuhumiwa kuandaa michakato hiyo wana uzoefu nalo
na yumkini ndiyo chachu ya mafanikio yao mpaka kufikia hatua hiyo waliofikia
sasa. Kama timu hizo zinauwezo wa kirasilimali wa kufanya uovu huo wote iweje
ishindwe kuwa na timu imara na ya ushindaji mpaka itegemee kutafuta wachezaji
wa timu pinzani kupata matokeo mazuri?
Timu yetu ndiyo timu pekee changa
miongoni mwa timu tano zinazoongoza msimamo wa ligi yetu kwa sasa,si hivyo tu
bali ndiyo timu pekee inayoundwa na wachezaji wengi wapya katika ulimwegu wa
soka na inayoundwa na Watanzania watupu kuanzia wachezaji,benchi la ufundi
pamoja na viongozi.Hii inathibisha kuwa kama taifa tunaweza kufanya kazi nzuri
bila kutegemea wachezaji toka nje baadhi yao wasiokuwa na tija.
Mpira ni ajira hatuna budi kuuratibu
vema ili kutoa nafasi inayostahili kwa vijana wetu ili kupunguza tatizola ajira
nchini lakini pia kutumia vipaji vyao kulipa taifa muonekano stahili.
Mamlaka zinazohusika hazina budi
kuanza kufuatilia na kuchukua hatua kali kwa baadhi ya timu zinzohusishwa na
upangaji wa matokeo ili kulinda heshima ya mchezo huo bila kuogopa uwezo wa
rasilimali na ushawishi wa timu hizo ili kuweka mazingira sawa ya ushindani.
E.E.Kimbe
KATIBU MKUU
MCC FC
9.04.2014
0 comments:
Post a Comment