SERIKALI
MKOANI MBEYA  IMEWATAKA WANANCHI KUCHUKUA
TAHADHALI YA UWEZEKANO WA KUWEPO KWA NYOKA MKUBWA KATIKA MTO WA SHULE YA
SEKONDARI MBEYA DAY
Hayo
yamebainishwa nae JOSEPH BUTUYUYU afisa mali ya asili mkoni mbeya alipokua
akizungumza na mwandishi wa habari hizi ofini kwake Butuyuyu amewataka wanachi
kuto dharau kuwepo kwa taarifa zanyoka mkubwa katika mapango ya mto unaopita
kati shule ya sekondali ya mbeya day
Ameongeza
kuwa Serikali imepata taarifa hizo na sasa tayali imechukua hatua ya kuiagiza
Halmashari ya jiji la mbeya kutafuta wataaram wanao weza kumtafuta nyoka huyo na
kisha kumpeleka katika ya hifadhi ifisi na tayali wataalamu hao kutoka chunya
na chalinze wamekwisha wasili na kuianza kazi hiyo mala moja
Kwa upande
wake mtaalam wa kumtafuta nyoka huyo Athumani Kenthi kutoka wilayani chunya
amethibisha kuwepo na dalili ya kuwepo kwa nyoka  kutokana na kuziona alma za njia anazopita na
kwamba wanaendelea kumtafua na kutoa wito kwa wwananchi watakao weza kumuona
kutoa taarifa katika maraka husika ili kuharakisha zoezi hilo.
Athumani
ameongezakuwa zoezi hilo ni gumu na kuna uwezekano wa kuchukua muda mrefu kutokana
na tabia ya nyoka huo kuto onekana mara kwa mara endapo kameza mzoga mkubwa
mpaka pale utakapo kua umeozesha Lakini hilo haliwakatishi tamaa mpaka atakapo
patikana.
Nae mmoja wa
wanafunzi wa shule ya mbeya sekondari inayo pakana na mto huo Gasto Mtega ameiomba
serikali kuchukua hatua za makusudi na za haraka kwani mpaka sasa wamekua
wakiishi kwa mashaka kutoka kuzagaa kwa habari  hizo ili kukabiliana nae kabla hajatoa madhara
kwa wanadamu. 
 
 
 
 
 
 
 
 
 
 
 
 
 
 
 
 
 
0 comments:
Post a Comment