SERIKALI
MKOANI MBEYA  IMEWATAKA WANANCHI KUCHUKUA
TAHADHALI YA UWEZEKANO WA KUWEPO KWA NYOKA MKUBWA KATIKA MTO WA SHULE YA
SEKONDARI MBEYA DAY
 Afisa mali ya asili mkoa wa Mbeya Joseph Butuyuyu akiongea na mwandishi wa blog hii ofisini kwake
muonekano wa sehemu inayosemekana kuwepo kwa chatu anae meza mbwa na mbuzi maeneo ya sabasabana shule ya Mbeya sekondari
Baadhi ya njia zinazotiliwa shaka kiwepo kwa chatu mkubwa lakini bado watu wanapita bila shaka hapa ni daraja linalopitisha watu kutokea kichochoro kati Tanrod na Mbeya Sekonari
 Moja ya maeneo ya mto unaodhaniwa kuwepo na chatu mkubwa
Vinjia vilivyopo pembezoni mwa mto na wigo wa mbeya sekondali vinavyotumika kupita watu pamoja na kuwepo kwa tahadhari ya nyoka mkubwa
 Hata hivyo shughuri za kuoga bado zinaendelea kwa wakazi waliopo karibu na mto huo
Wananchi bado wanatumia daraja linalo wavusha kutoka jakaranda kwenda katika makaburi ya sabasaba
Wanafunzi wa Mbeya sekondari wanaendelea na shughuri zao japo nje ya wigo huo niko anakosakwa chatu
Katika mapolomoko haya kuna mti mkubwa mkavu inasemekana ndipo yalipo makazi ya chatu huyo
Mtaala wa kukamata nyoka Mazoea Hamisi toka Chalinze akiwajibika kumtafuta chatu Huyo
Wataalam wa kukamata nyoka wamefanikiwa kumkata nyoka wa kijani
Mazoea alikosea kumkamata nyoka aliruka na kumgonga kidole gumba
Mtaalamu wa kukamata nyoka akifanikiwa kumdhiditi tena nyoka huyo
Hapa akitoa meno ya nyoka kisha kujitibia kwa dawa zake
 kazi ya kusaka nyoka huyo inaendelea kwa kuzama mapangoni na mapolini
Hatimaye tumaini linaongezeka baada ya kumnasa mmoja wa chatu hao ambao inasemekana ni mtoto na kuna uwezekano wa kuwepo wazazi wake
Tuna mshukuru mchina kwa kutuletea simu zenye kamera na hawa ni wakazi wa jiji la mbeya waliojitokeza kumuona nyoka huyo
                                    Habari kamili
SERIKALI
MKOANI MBEYA  IMEWATAKA WANANCHI KUCHUKUA
TAHADHALI YA UWEZEKANO WA KUWEPO KWA NYOKA MKUBWA KATIKA MTO WA SHULE YA
SEKONDARI MBEYA DAY
Hayo
yamebainishwa nae JOSEPH BUTUYUYU afisa mali ya asili mkoni mbeya alipokua
akizungumza na mwandishi wa habari hizi ofini kwake, Butuyuyu amewataka wanachi
kuto dharau kuwepo kwa taarifa zanyoka mkubwa katika mapango ya mto unaopita
kati shule ya sekondali ya mbeya day
Ameongeza
kuwa Serikali imepata taarifa hizo na sasa tayali imechukua hatua ya kuiagiza
Halmashari ya jiji la mbeya kutafuta wataaram wanao weza kumtafuta nyoka huyo
na kisha kumpeleka katika ya hifadhi ifisi na tayali wataalamu hao kutoka
chunya na chalinze wamekwisha wasili na kuianza kazi hiyo mala moja
Kwa upande
wake mtaalam wa kumtafuta nyoka huyo Athumani Kenthi kutoka wilayani chunya
amethibisha kuwepo na dalili ya kuwepo kwa nyoka  kutokana na kuziona alma za njia anazopita na
kwamba wanaendelea kumtafua na kutoa wito kwa wwananchi watakao weza kumuona
kutoa taarifa katika maraka husika ili kuharakisha zoezi hilo.
Athumani
ameongezakuwa zoezi hilo ni gumu na kuna uwezekano wa kuchukua muda mrefu
kutokana na tabia ya nyoka huo kuto onekana mara kwa mara endapo kameza mzoga
mkubwa mpaka pale utakapo kua umeozesha Lakini hilo haliwakatishi tamaa mpaka
atakapo patikana.
Nae mmoja wa
wanafunzi wa shule ya mbeya sekondari inayo pakana na mto huo Gasto Mtega
ameiomba serikali kuchukua hatua za makusudi na za haraka kwani mpaka sasa
wamekua wakiishi kwa mashaka kutoka kuzagaa kwa habari  hizo ili kukabiliana nae kabla hajatoa
madhara kwa wanadamu. 
                                        Mwisho 
 












































 
 
 
 
 
 
 
 
 
 
 
 
 
 
 
 
0 comments:
Post a Comment